Wednesday, April 27, 2022

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI KUTOA SH. 15 MILIONI KUTANGA UTALII KIMBWI

Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi, Winfrida Funto akizungumza na washiriki wa Kongamano la Vijana la Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika jana katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi jana. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akizungumza kwenye kongamano hilo. 

Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Ikungi Kennan Kidanka alitoa mada iliyohusu Maadili ya Kitaifa na Uzalendo.
Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Julius Method akizungumza kwenye kongamano hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ikungi wakishiriki katika kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka Shirika la SEMA, Nice Daudi, akitoa mada iliyohusu Historia ya Muungano na Faida zake.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikungi wakiwa kwenye kongamano hilo.
Mshereheshaji wa kongamano hilo Mwalimu Baraka Shifie wa Shule ya Sekondari ya Ikungi akifanya vitu vyake.
Mwanafunzi Kairin Mashanjara wa Shule ya Sekondari Ikungi akichangia jambo wakati wa majadiliano.
Mwanafunzi Leah Kibaja akichangia jambo.
Michango mbalimbali ikitolewa kwenye kongamano hilo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Kaweso Gadiel akitoa mada iliyohusu Fursa ya Mikopo na Taratibu zake.
Afisa Miradi wa Taasisi ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida, Rebeca Wellia akitoa mada kuhusu Uthubutu wa Vijana katika Fursa zinazokuja.
Rilper Swedi akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Mwanafunzi Sarah Peter kutoka Shule ya Sekondari Ikungi akizungumza kwenye kongamano hilo.
Taus Mwiko akizungumzia umuhimu wa utamaduni katika jamii.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ufyatuaji wa tofari cha Puma, Paul Mbua akichangia jambo kwenye kongamano hilo hasa kuhusu utoaji wa mikopo.

Na Dotto Mwaibale, Ikungi

HALMASHAURI ya Wilaya Ikungi imeahidi kutoa Sh.15 Milioni kwa vijana watakaoamua kujiunga pamoja na kuutangaza utalii katika eneo la utalii la Kimbwi lililopo wilayani humo mkoani Singida.
Hayoyalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Justice Kijazi wakati akizungumza na vijana katika Kongamano la 58 la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar liliofanyika wilayani humo jana.

"Halmashauri yetu ipo tayari kutoa Sh.15 Milioni kwa vijana au mtu yeyote atakayekuwa tayari kutangaza utalii na utamaduni wetu katika eneo la Kimbwi lenye historia ya kipekee" alisema Kijazi.

Kijazi aliwataka vijana katika wilaya hiyo kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji katika maeneneo ya utalii, ufugaji, kilimo, michezo na utamaduni na nyingine nyingi zilizopo.

Alisema katika wilaya hiyo kunawawekezaji wa kubwa wataanza kuwekeza katika viwanda vya kuzindika nyama,kilimo na miradi mingine hivyo vijana wametakiwa kuchangamkia fursa hiyo.

"Vijana ni Taifa la leo hivyo mnatakiwa kuwa waajiri na si kuajiriwa hapa nchini idadi ya watu ni zaidiya Milioni 60 na Serikali inauwezo wa kuajiri watu 2000 tu hivyo nawaombeni ondoeni dhana ya kutaka kuajiriiwa bali jielekezeni katika uwekezaji wa miradi" alisema Kijazi.

Aidha Kijazi aliwataka vijana kuwa waaminifu pale wanapopewa mikopo na Serikali kwani imeonesha kutorejesha mikopo ukilinganisha na wanawake ambao kutokana na kuwa waaminifu wamekuwa wakiendelea kukopeshwa.

Kijazi pia alihimiza kufanyika kwa makongamano ya vijana wilayani humo ambayo yataibua mambo mbalimbali ya maendeleo lakini akatoa angalizo kuwa waratibu wa makongamano hayo wasiwapangie cha kuwaambia bali wao wawaambie kile wanachotaka.

Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Winfrida Funto ambaye alikuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo aliwataka vijana kuwa wazalendo wa nchi na kuulinda Muungano wetu ambao ni tunu ya Taifa.
Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale bado muungano umeendelea kuimarika kutokana na kuzibaini na kuzitafutia ufumbuzi hali inaoufanya uendelee kustawi ambapo aliwata vijana kuendelea kuuenzi.

Alitaja baadhi ya faida ya Muungano kuwa ni kudumu kwa mshikamano wa kitaifa, kuimarika kwa ulinzi na usalama, kukua kwa shughuli za kibiashara na kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kama ardhi na bahari na kufurahia matunda ya uraia wa nchi moja na wananchi kuishi sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muingiliano wa utamadu kama chakula, mavazi, mitizamo, maarifa, maadili na  kuoana.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilitolewa kama fursa zilizopo katika wilaya hiyo ambayo iliwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Justice Kijazi, Historia ya Muungano na faida zake iliyotolewa na Mwakilishi kutoka Shirika la SEMA, Nice Daudi, Fursa za mikopo na taratibu zake, iliyowasilishwa na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Kaweso Gadiel,Maadili ya Kitaifa na Uzalendo iliyotolewa na Afisa Utamaduni wa wilaya hiyo Kennan Kidanka na mada iliyohusu Uthubutu wa Vijana katika Fursa zinazokuja iliyotolewa na Afisa Miradi wa Taasisi ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida, Rebecca Wellia.

Aidha washiriki wa kongamano ambao walikuwa ni wananchi, wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Ikungi na viongozi mbalimbali walipata fursa ya kuuliza maswali na kufanya majadiliano.

No comments:

Post a Comment