Tuesday, March 15, 2022

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe pamoja na Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

 

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Waziri akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Malawi Humphrey Polepole wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba Waziri na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Waziri Kindamba mara baada ya hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole mara baada ya hafla fupi ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment