Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza na Wazee wasiojiweza wanaoishi katika Makazi ya Wazee Bukumbi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake kwenye Makazi hayo kufuatilia utendaji kazi na huduma zinazotolewa kwa wazee.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akisalimiana na Wazee wanaoishi katika Makazi ya Wazee Bukumbi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake kwenye Makazi hayo kufuatilia utendaji kazi na huduma zinazotolewa kwa wazee.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akikagua mradi wa maji katika Makazi ya Wazee wasiojiweza ya Bukumbi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake kwenye Makazi hayo kufuatilia utendaji kazi na huduma zinazotolewa kwa wazee.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akiwapa kinywaji cha soda baadhi ya Wazee wanaoishi katika Makazi ya Wazee ya Bukumbi mkoani Mwanza wakati wa ziara yake kwenye Makazi hayo kufuatilia utendaji kazi na huduma zinazotolewa kwa wazee.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
Na WMJJWM- Mwanza
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum Amon Mpanju ameitaka jamii kuwalinda na kuwalea Wazee kwani ni hazina kubwa kwa jamii katika maendeleo.
Mpanju ameyasema hayo mkoani Mwanza alipotembelea Makazi ya Wazee Bukumbi yaliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza yenye lengo la kukagua huduma zinazotolewa katika Makazi hayo.
Ameongeza kuwa suala la kulea Wazee ni la kila mtu hivyo amewataka wadau na wanajamii kuunga mkono jitihada za Wizara kuwatembelea na kuwasaidia Wazee katika Makazi na sehemu mbalimbali nchini.
Aidha amemtaka Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutenga ya maeneo ya kufanyia mazoezi na michezo mbalimbali ya kuwachangamsha Wazee hao wakiwapo katika Makazi hayo.
Akitoa taarifa ya Makazi hayo Afisa Mfawidhi Jonas Tarimo amesema kuwa wameshirikiana na wadau kutoka Shirika la Desk and Chair kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Makazi hayo hivyo kurahisisha huduma mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa mbogamboga.
Akizungumza kwa niaba ya Wazee wa Makazi ya Wazee John Nguku ameishukuru Wizara kwa kuwahudumia katika Makazi hayo na kuomba kupatiwa usafiri wa uhakika ili uwasaidie kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Desk and Chair Sibtain Meghjee amesema Shirika lake litaendelea kusaidia katika maboresho ya Makazi hayo na kusaidia upatikanaji wa huduma ya Afya kwa kuwapatia Kadi za Bima ya Afya Wazee wanaoishi katika Makazi hayo.
No comments:
Post a Comment