Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wa tatu kutoka kushoto , akiwa na mkuu wa wilaya ya ikungi Jerry Muro na wafanyakazi wa wa kampuni ya uchimbaji madini ya SHANTA GOLD alipofanya ziara kukagua miradi mbambali.
Wafanyakazi wa shanta gold wakiendelea na kazi , mkuu wa mkoa na akishuhudia kazi inavyofanyika .
Miongoni mwa madarasa ya shule ya msingi yaliyojengwa na shanta gold ambayo mkuu wa mkoa dkt binilith mahenge aliikagua kwenye ziara yake.
Meneja mradi was hanta gold Kundael Mtiro akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa
Mkuu wa mkoa akizungumza wafanyakazi was hanta gold na wachimbaji katika eneo mojawapo la uchimbaji wa dhahabu.
Na Hamis Hussein – Singida
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge
amewashauri wawekezaji mkoani hapa w kushirikiana na Halmashauri za
Wilaya wakati wa kuanzisha miradi ya Maendeleo ya Kijamii (Community Socially
Responsibility – CSR) ili kuwa na tija kweenye miradi hio na kuepuka matumizi
makubwa ya fedha wakati wa utekelezaji wake.
Akizungmza
na wafanyakazi wa machimbo ya madini ya dhahabu yanayochimbwa na kampuni ya
Shanta Gold iliyopo kijiji cha Mang’onyi wilayani Ikungi alipofanya ziara
kukagua mradi huo Mkuu huyo wa mkoa Dkt. Mahenge mbapo alisema kuwa miradi yote inayoanzishwa na wawekezaji ipitie
katika Halmashauri za Wilaya ambazo zinafahamu mahitaji ya wahusika na gharama halisi za ujenzi katika maeneo hayo.
Dkt.
Mahenge alitolea mfano kwa madarasa
yalikamilika hivi karibuni kupitia fedha za uviko alisema kuwa kila darasa
liligharimu kiasi cha shilingi milioni 20, ikilinganishwa na madarasa
yaliyojengwa na Shanta Gold ambayo yamegharimu Tsh.milioni 28 kwa kila darasa.
“Kama mradi huu mngeshirikisha
Halmashauri kwa kiasi kikubwa mngetumia Force Account na mgepata wakandarasi wa
bei ndogo na fedha zingebaki zikafanya maendeleo mengine katika jamii.
Niwashauri mshirikiane ipasavyo na Halmashauri kupanga aina ya miradi mnayotaka
kuipeleka kwa jamii”. alisema Dkt. Mahenge.
Mkuu
huyo wa mkoa mwenye uzoefu mkubwa serikalini akaipongeza Kampuni ya shanta gold mining kutumia zaidi ya Milioni 190 kupelekea jamii huduma
ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na uchimbaji wa visima vya maji huduma
ambazo zinafaidisha vijiji vya Mang’onyi, Sambaru, Mlumbi, Tupendane na Mwau.
Aidha,
Dkt. Mahenge akaitaka jamii inayozunguka mgodi huo kutumia fursa na kuwa
wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku na mama lishe
pamoja na kuomba ajira katika kampuni hiyo kwa kuwa kadri mradi unavyokuwa
ndivyo mahitaji yatakavyoongezeka.
Meneja
wa Mradi huo kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya Shanta gold Kundael Mtiro wakati akiwasilisha taarifa ya
mradi amesema mpaka kufikia sasa mradi ulitakiwa kufikia asilimia 46.14 katika
utekelezaji wake lakini kwa sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo mpaka sasa
utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 43.62 .
Ameongeza
kuwa kufikia June, 2022 mradi utakuwa
unakamilisha robo ya nne ya mwaka ambapo
wanategemea kwamba utakuwa umekamilika kwani mabomba yameshasimika katika maeno
yote yanayohusika pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa ofisi na makazi
umekamilika kwa asiliami 80.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akiwa miongozni mwa viongozi walioongozana na
mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo akataja jinsi mgodi huo utakavyowanufaisha watu
wanauzunguka mgodi huo hususani wakazi wa ikungi , Singida na taifa kwa ujumla
ambapo utasisimua sekta nyingine za elimu barabara, zahanati na wananchi kupata
ajira.
No comments:
Post a Comment