Thursday, December 2, 2021

NCHINI HISPANIA : TANZANIA YAPONGEZWA KIMATAIFA KATIKA MASUALA YA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( katikati) akiwa Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Ufaransa, Mhe.Samwel Shelukindo ( kulia)  pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi (kushoto)  wakifuatlia  Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa  Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa  jana rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (  wa nne  kulia ) akiwa Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye makazi yake ya kudumu nchini Ufaransa, Mhe.Samwel Shelukindo ( wa kwanza kulia)   akiwakabidhi zawadi mbalimbali Watendaji Wakuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii  (UNWTO) kanda ya Afrika  Elsia Grancourt ( wa tatu kulia)  pamoja na  Natalia Bayona ( wa pili kushoto)  katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa  Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa  jana rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi na kwanza kushoto ni Afisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Lily Fungamtama
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (  wa nne  kulia )  akiwakabidhi zawadi ya tisheti  Watendaji Wakuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii  (UNWTO) kanda ya Afrika  Elsia Grancourt ( kulia)  pamoja na  Natalia Bayona ( kushoto)  katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa  Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa  leo rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi na kwanza kushoto ni Afisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania, Lily Fungamtama
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (  katikati ) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Richie Wandwi ( wa kwanza kulia) wakimsiliza Mtumishi wa Ubalozi wa ujerumani nchini HIspania, Jacobr Nsihkl  akilezea maeneo ya vivutio vya utalii alivyotembelea mwezi uliopita wakati alipokuja nchini Tanzania  katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa  Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) uliofunguliwa  jana rasmi na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania.
Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololkashvill akizungumza wakati alipokuwa akifungua  Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa 24 wa  Shirika la Umoja wa Kimataifa linaloshughulikia Masuala ya Utalii Duniani ( UNWTO) unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Madrid nchini Hispania ambapo ametumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania kufanikisha  kufanya Onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki lililofanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Arusha kwa  lengo la kutangaza utalii katika nchi za Jumuiya za ukanda huo

NA MWANDISHI WETU MAALUM MADRIDI, HISPANIA
 
Tanzania yapongezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO) kwa namna ambavyo ilifanikisha  kufanya Onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki lililofanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Arusha lililokuwa na   lengo la kutangza utalii katika nchi za Jumuiya za ukanda huo 

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Utalii Duniani (UNWTO), Zurab Pololkashvir wakati akitaja baadhi ya nchi za Afrika ambazo licha ya changamoto ya ugonjwa wa Korona lakini zimeendelea kufanya vizuri katika suala la utalii 

 Ameyasema hayo  mapema jana wakati alipokuwa akitaja baadhi ya mafanikio yake katika Uongozi wake tangu  alipochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa UNWTO  katika  siku ya pili  ya  Mkutano Mkuu wa 24 wa UNWTO ulipoanza.

Amesema Tanzania ni moja kati ya nchi katika bara la Afrika zinazochipukia katika kuhakikisha sekta ya utalii inafanya vizuri kwa kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa ajili ya kutangaza vivutio vyake vya utalii

Ametaja Onesho la kwanza la Utalii la Afrika Mashariki (EARTE) kuwa Tanzania imeonesha ukomavu na ujasiri  wa hali ya juu katika kulifanya kwa mafanikio makubwa Onesho lile licha ya kuwa na muda mfupi wa maandalizi na uwepo wa changamoto a ugonjwa UVIKO -19

” Kati ya nchi za Afrika ninazoziona zinakwenda kuongoza kimapato kwa kuifanya sekta ya utalii kuwa namba moja huwezi kuiacha kuitaja Tanzania ” am so proud of you Tanzania” alisema  Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab

Akizingumzia pongezi hizo,  Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab kwa kuonna na kukubali jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania katika kuhakikisha sekta ya utalii inaendelea kufanya vizuri kimapato
  ”Tumepongezwa kwa namna ambavyo tumeweza kufanya onesho la kwanza la utalii katika nchi za Afrika Mashariki. Sisi tuliona dogo, lakini wenzetu huku katika nyanja za kimataifa waliliona kubwa ” alisema  Dkt. Ndumbaro

Amesema Onesho la EARTE pamoja na   mkutano huu wa UNWTO kwa nchi ya Tanzania ni fursa ya skuweza kutangaza utalii, lakini kama fursa ya kuwavuta wenzetu watalii waje pia nchini Tanzania katika kuwekeza kwenye sekta ya utalii

Dkt. Ndumbaro amesema pongezi hizo zinatia moyo yta kuongeza kasi zaidi katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ” Tumepongezwa na nimesema kwamba kumbe kweli watanzania wanaweza kufanya mikutano kwa kiwango kikubwa zaidi’’ alisema Dkt. Ndumbaro.

Kupitia Pongezi hizo, Dkt.Ndumbaro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan  kwa Ushirikiano mkubwa anaoupata kutoka kwake huku akitaja Kampeni maalum cha kutangaza utalii wa kupitia kipindi cha ‘ Royal Tour’ aliyoiasisi yeye mwenyewe kuwa hali inampa nguvu zaidi katika kutangza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi

Katika hatua nyingine Dkt. Ndumbaro katika mkutano huo wa siku nne unaoendelea kufanyika katika Jiji la  Madrid anatumia fursa hiyo ya kushiriki katika kuwaalika Viongozi mbalimbali wa Kidunia Mawaziri wa Utalii pamoj na Wataalamu mbalimbali wa  utangazaji na masuala ya utalii katika kuwaalika kushiriki katika Mkuu wa Utalii wa Kanda ya Afrika ambapo Tanzania anataraji kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo utakafanyika Oktoba 6 hadi 8 mwaka 2022

No comments:

Post a Comment