Wednesday, December 1, 2021

MAKALA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM

 




Na Nathaniel Limu – SINGIDA

 

Unaweza ukawa unafahamu kuwa CHAMA cha mapinduzi (CCM) ni  kama chama tawala nchini Tanzania Lakini unapaswa kufahamu CCM ni chama cha pili ambacho kimekaa madarakani kwa muda murefu  baada ya chama cha TRUE WHIG PARTY TWP cha Liberia kwa ukanda wa afrika kilichoanzishwa 1869 . CCM siyo tu chama tawala nchini Tanzania bali ni cha ambacho kimedumu madarakani kwa miongo mingi na hakijapata misuko suko ya kutishia uhai wake.

Chama hiki kilichoasisiwa na hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kimezaliwa mapema katika miaka ya 1977 ikiwa ni zao la muungano chama cha TANU ambacho kilikuwa upande wa Tanganyika na AFRO- SHIRAZI PARTY ASP Kutoka visiwani Zanzibar kisha kuungana na kuunda chama kimoja ambacho ni Chama Cha Mapinduzi CCM kinachotambuliwa hadi sasa vizazi na vizazi ingawa mwaasisi alikuwa ni baba wa taifa Hayati Mwalimu Julias Nyerere alieU ilikomboa  nchi kutoka  mikononi mwa wakoloni Waingereza.

CCM katika chaguzi mbalimbali ikiwemo chaguzi kuu, kimekuwa kikigaragaza vyama vya upinzani na Ushindi mnono wa CCM unatokana na kuwa na ilani thabiti ya uchaguzi, inayo watetea  maslahi ya wananchi hususani wale  wanyonge kupitia viongozi wenye utu utakumba Mwenyekiti wa kwanza wa ccm Mwalimu nyerere ni moja ya viongozi waliotengeneza msingi mizuri ya viongozi wa chama na serikali ambao wamekuwa ni kichocheo cha utekelezaji wa ilani za chama hiki kikongwe.

Kupitia ilani hiyo, CCM imekuwa ikishinda mapema asubuhi. Katika chaguzi zote, ushindi wa CCM haujawahi kutiliwa mashaka. Hali hiyo imekuwa ikiwapa jeuri wenye chama hicho, wanachama na mashabiki wake. Hili kundi limekuwa likiwatambia watani zao (Upinzani) kwa wimbo unaomalizia kwamba ‘Wataisoma namba’  pindi wanapopanda katika majukwaa ya kisiasa , amewahi kusema alikuwa mwenezi wa ccm 2015-2020 ambeye kwa sasa ni Mbunge Mteule Ndugu Humphey Polepole  kuwa ccm wanachapa kazi wapinzani wamebaki na kauli ya kuminywa kwa demokrasia lakini hawana hoja ya msingi ndio maana kwa sasa wananshindwa kihalali na CCM.

Jeuri nyingine ya CCM, ni ile ya kuunda serikali makini na inayowajali zaidi wanyonge. Wana CCM na baadhi ya wasio wana CCM, wameendelea kukunwa na utekelezaji wa ilani hizo. Pia wanakunwa na utumbuaji wa viongozi wasio waadilifu au wanaojinufaisha kupitia mali ya umma. 

 

Uchaguzi mkuu uliopita wa 2020, CCM mkoa wa Singida ilikomba karibu nafasi zote za udiwani,ubunge na Rais alipata kura za kutosha huku ikiwaacha wapinzani wake wakigawana kura kiduchu mno.Jimbo la Singida mashariki lililokuwa mikononi mwa CHADEMA,lilirejeshwa kwa kishido mikononi mwa CCM.

CCM ya sasa ya awamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imejiongeza kwa mambo mengi ya maendeleo.Hasa katika kuondoa kero na changamoto zinazowakabili wananchi wanyonge.Kujiongeza huko,ni pamoja na   kuziagiza kamati za siasa ngazi ya mkoa, kutembelea na kukagua  miradi ya maendeleo ya wananchi mara kwa mara. Ukaguzi huo ujikite kubaini iwapo utekelezaji wa miradi hiyo, utafanana na thamani ya fedha zilizotumika, na si vinginevyo.


kamati ya siasa mkoa wa Singida pamoja na kufanya vizuri kwenye kaguzi zake, na yenyewe imejiongeza. Imejiongeza kwa kuziagiza kamati za siasa wilaya, nazo ziwajibike katika kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya wananchi. Endapo zitabaini ubadhilifu         wo wote,wawajibishe wahusika.

Mwenyekiti CCM mkoa Alhaji Juma Kilimba, amesema kaguzi za kamati za siasa wilaya, zina faida nyingi. Amefafanua zaidi kwamba faida za kaguzi hizo za mkoa na wilaya, ni pamoja na kuchukua hatua mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Mapema julai mwaka huu (2021) mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge, aliitisha kikao maalumu kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM, katika kipindi cha Julai mwaka 2020 hadi juni mwaka huu (2021). kikao hicho kimeweka rekodi ya kuhudhuriwa na  baadhi ya viongozi wa CCM na waalikwa mbali mbali.

Katika utangulizi wake mkuu huyo wa mkoa amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, ni tamko na ahadi maalumu zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020.

Amesema CCM kilimteua/mchagua Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli, kuwa mgombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati Rais wa sasa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan, alikuwa mgombea mwenza.

kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, CCM ilitoa ahadi za kuendelea kulinda uhuru, kuimarisha Muungano, kulinda Tunu. Tunu hizo za kitaifa ni pamoja na falsafa ya mwenge wa uhuru. Vile vile kuendelea kujenga taifa imara linalojitegemea kiuchumi na kisiasa  “amesema Dk. Mahenge.

Ameongeza kwamba utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi wa dira ya taifa ya maendeleo 2025.

 

Aidha, amesema unaenda sambamba na mpango wa maendeleo ya taifa (2021/2022-2025/2026. Na mwongozo wa mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O and OD).Dk. Mahenge alisema

 “Na vile vile Serikali imeendelea kuboresha miundombinu, kupanga matumizi bora ya ardhi, utoaji huduma bora za kijamii zinazojumuisha elimu,afya na maji. Kuimarishamakusanyo ya mapato ya ndani ya mamlaka za Serikali za mitaa. Kama hiyo haitoshi, tumeimarisha masuala ya utawala bora, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi,” amefafanua zaidi Dk. Mahenge ambaye ameahidi atahakikisha Mkoa wa Singida, unapaa kimaendeleo.

ILANI YA CHAMA KUHUSU MAENDELEO KWA MKOA WA SINGIDA

‘HALIYA KIUCHUMI

Ni wazi ilani ya ccm inatekelezwa kitaifa itakubukwa katika kitabu cha ilani katika uchaguzi wa mwaka 2020 kikiwa na kurasa zaidi ya 300 kilibainisha mambo mbalimbali ya maendeleo , Dk. Binilith Mahenge Mkuu wa mkoa wa singida, alisema asilimia 80 ya wananchi mkoani humo, wanajishughulisha na shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi ambapo kwa sasa usalama ndani ya mkoa, umeimarika na kuwezesha wananchi kutekeleza majukumu yao ya kiuchumi na kijamii kwa amani na utulivu mkubwa.

“Hali hii imewezesha hali ya uchumi kuwa na mafanikio mbalimbali. Mafanikio hayo ni pamoja na kukua kwa pato la mkoa (GDP) kutoka shilingi trioni 2.6 kwa mwaka 2019 hadi kufikia shilingi trioni 2.7 mwaka 2020. Na kukua kwa pato la wastani la kila mtu kwa mkoa wa Singida kutoka shilingi 1.5 milioni mwaka 2019 hadi kufikia shilingi 1.6 milioni kwa mwaka 2020”. amesema.

Utekelezaji wa ilani umeoneka kuwa chanya na inathibitishwa na Dk. Mahenge ambaye ametaja maboresho ya matumizi ya ardhi vipande 10,481 kati ya lengo la vipande 3,500 ambayo ni sawa na asilimia 299 ni miongoni mwa mambo yalitekelezwa kiuchumi kwenye ilani hiyo.

‘MIUNDOMBINU’

Mtoto au Mjukuu wangu akiamka usingizini na kuniuliza kwa CCM imekaa Madarakani muda mrefu Nitamkumbusha tu msemo wa waswahili usemao ‘Wali wa kushiba utauona kwenye sahani ‘ CCM ni chama ambacho kinafanya maandalizi kwa kizazi kijacho angalia mionombinu ya shule , afya, barabara . mkoa wa singida ni mwiongoni mwa watekelezaji wazuri wa ilani ya ccm .Dkt. Mahenge Amesema wamepokea jumla ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya kugharamia ahadi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami  kuanzia Sabasaba mjini Singida- Sepuka –Ndago-Kizaga yenye urefu  wa kilometa 77.


Kama,hiyo haitoshi Desemba 1. 2021 mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge ameshiriki Utiaji saini Mkataba wa marekebisho ya barabara  kwa halmashauri zote Saba (7)  za Mkoani hapa kati ya wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA mkoa wa singida na wakandarasi walishinda tuzo  ya kazi mkataba wenye thamani ya Sh. Bilioni 12.6.



Utasema nini juu yaujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 600 kupitia fedha za mkopo kutoka IMF kwaajili ya kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa wa Uviko 19. Kweli wanasema wasemaji ‘ Ukinuna uwe na sababu’

‘SEKTA YA AFYA’

Hebu jiulize fedha zilizotengwa za ujenzi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida inayojengwa mtaa wa mandewa ambapo sh. Bilioni 5.9 zilizotengwa na ujenzi umefikia asilimia 70 kwa awamu kwanza.uundwaji wa kamati mbalimbali zitakazotekeleza maagizo ya waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima  Kusimamia masuala mbalimbali ikiwemo dawa , uchangiaji Damu matumizi ya fedha .


Tusisahau basi jipya kubwa litakalo wasafirisha wafanyakazi kwenda kuwahudumia wangojwa katika kuboresha huduma. Kutaja machache.


 KILIMO NA MAZAO YA KIMKAKATI’

Kupitia ilani ya chama singida inayo mazao ya kimkakati ambayo lengo lake ni kuokomboa jamii kiuchumi , mazo hayo ni pamoja na,

     i.        KOROSHO - Ambapo mkoa  umefanikiwa kutekeleza ahadi ya kutoa miche ya mikorosho 202,970. miche 82.008 imepelekwa Halmashauri ya Itigi, na miche mingine 120,962 imepelekwa Halmashauri ya Manyoni.


   ii.        ALIZETI- Dk.Mahenge anasema mkoa umeandaa mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti.Ahadi ya utekelezaji huo utatekelezwa na Halmashauri zote saba kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo.Anasema mkakati huo ni pamoja na kupanua/kuongeza eneo litakalolimwa zao la alizeti.Jumla ya Ekari 596,909 zitalimwa ikilinganishwa na ekari 205,000 za msimu wa 2021. Aidha,anasema watahakikisha mbegu bora zinapatikana na kutumika katika uzalishaji kwa kukidhi mahitaji ambayo kwa mkoa,ni tani 1,194.

  iii.        KILIMO CHA UMWAGILIAJI - Mkuu huyo wa mkoa,anasema mkoa una jumla ya hekta 2,060.5 zinalimwa kilimo cha umwagiliaji.Pia mkoa una skimu zenye uhakika wa kuhudumia misimu miwili kwa mwaka.


“Tutaendelea kutoa elimu kwa wakulima 2,036 kati ya 7,039 kuhusu kilimo bora.Vile vile tutahimiza utunzaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji kwenye skimu ya Itagata-Itigi.Jumla ya ekari 24 zimeongezwa na kufanya jumla ya ekari 219 zenye miundo mbinu ya maji,” anasema.

MAPAMBANO DHIDI YA GONJWA HATARI LA CORONA.

Mkuu huyo wa mkoa,ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea,wanapata  Chanjo ambayo ni njia yenye ufanisi katika kukinga na kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa  huo.

Anasema Chanjo ya CORONA inawezesha kinga ya mwili kupambana na virusi vya CORONA pale mtu anapoambukizwa. Dk.Mahenge anasema Chanjo ya CORONA inatolewa bila malipo na inapatikana nchi nzima katika Hospitali na Vituo maalum.

Hadi sasa kupiti wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsis na watoto ,kuna aina nne za Chanjo ambazo zimeidhinishwa kutumika nchini kwa ajili ya kinga ya  CORONA,ambazo ni Johnson and Johnson,Pfizer,moderna and Sinovac & Sinopharm.

Haya ni machache kati ya mengi ambayo yanatekelezwa na yataendelea kutekelezwa na chama hiki kikongwe ambacho kila kada alikulia hapo huwa hatamani kutoka kabisa , wapo wanaojaribu kwenda kutembea vyama vingine vya upinzani lakini wakiona matunda na raha wanayoipata hurudi hadi wapinzani hujongea kule kwa wacha waisome namba eee ccm mbele kwa mbele, mwisho wa siku ‘Utamu wa Kidonda Hummaliza Inzi’. Asanteni sana Tusherekee kwa amani miaka 60 ya Uhuru wetu . Kazi iendelee hadi wakati mwingine tena.

 



 

No comments:

Post a Comment