Thursday, November 25, 2021

FPTC YATOA MAFUNZO UTETEZI WA HAKI ZA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM


Na, Nathaniel Limu - Singida 

KANISA  la Pentekoste Tanzania (FPCT) Singida mjini kati, kupitia kitengo chake cha Singida,Town Centre  Church (STCC),  limetoa mafunzo juu ya mpango kazi wa utetezi wa haki za watoto wenye mahitaji maalum, ili kuwajengea uwezo wajumbe wa mradi wa Elimu jumuishi, waweze kutekeleza  majukumu yao kwa ufanisi.


Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la  Singida,Town Centre  Church (STCC), yalitolewa na shirika la International Aid services (IAS) la Dermark kwa njia ya  mtandao yaani Zoom.

Mkurugenzi wa shirika la IAS, Jovben Madsen, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo, kwa watu wenye uwezo wa kutoa sauti, ili waweze kupaza sauti kwa niaba ya watu wasio na sauti wweze kupata haki zao za msingi.


watoto na hata baadhi ya watu wazima,bado  wanaendelea kudhulumiwa haki zao.Watu wazima wameathirika kiuchumi.Pia wanafanyiwa  vitendo vya unyanyasaji mbavyo vipo kinyume na haki za kibinadamu. Mbaya zaidi  hawana uwezo wa  kutetea haki zao. Amefafanua mkurugenzi wa IAS Madsen

Mkurugenzi huyo ameongeza  kwamba watu wasio na uwezo wa kujisemea au kutetea haki zao, wapo sehemu mbalimbali duniani. Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, alinukuu kifungu kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Methali 31-9 (kifungu cha nane na tisa). Nukuu inasema “Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu, uwatetee watu wote walioachwa peke yao”.

Mkurugenzi Madsen, amefarijika kwa kitendo cha kiongozi wa serikali ngazi ya juu mkoani Singida,Fatuma Malenga, kuwa ni miongoni  mwa viongozi wa mradi wa elimu jumuishi na mchango wake utakuwa na tija zaidi.



Katika hatua nyingine, mratibu wa mipango shirika la IAS Katja, amesema katika kitabu kitakatifu cha Biblia, nacho kimeainisha kwamba baadhi ya watu wenye madaraka, nao wanatumia nafasi  hizo, kunyanyasa watu wasio na sauti.  Kwani katika biblia takatifu  Isaya 3 mstari wa 14, nukuu yake inasema “Bwana ataingia katika kuwahukumu wazee na watu wake na wakuu wao, ‘ninyi ndio mliokula shamba la mzabibu, vitu mlivyowateka maskini, vii ndani ya nyumba zenu”. 

Kuhusu changamoto zinazojitokeza,Katja ameshauri mjumbe yeyote wa mradi endapo atakabiliwa na changamoto ya aina yo yote, asiikabili peke yake,ashirikishe wenzake.

Wakati huo huo,mjumbe wa shirika la walemavu SHIVYAWATA manispaa ya Singida,Idd Hassan,amesema mafunzo hayo yalikuwa mazuri, na kwa vyo vyote yataleta matokeo chanya na kutumia fursa hiyo kuiomba serikali ngazi mbalimbali kuangalia uwezekano wa kutunga sheria ndogo ndogo, zitakazowadhibiti wazazi wanaoficha watoto wao wenye ulemavu kupata haki zao.


“Naziomba  mamlaka na wadau wengine  kusaidia kujenga miundo mbinu rafiki  katika maeneo ya shule,vyuo na sehemu zingine.Ili kuwaondolea usumbufu/kero watu wenye ulemavu.Na vile vile serikali iangalie uwezekano wa kumaliza uhaba mkubwa wa walimu wa viziwi”,alisema Hassan.


No comments:

Post a Comment