Timu ya kata ya Shibula imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali katika mashindano ya mpira wa miguu ya Angeline Jimbo Cup 2021 yanayoendeshwa na kufadhiliwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula katika mchezo wake dhidi ya Timu ya kata ya Buswelu uliochezwa Leo katika viwanja vya shule ya msingi Sabasaba kwa mikwaju ya penati baada ya tamati ya dakika tisini kutoka sare ya kufungana goli moja kwa moja.
Akizungumza mara baada ya kuisha kwa mchezo huo, Kocha wa timu ya kata ya Shibula Benedicto Henelick ametamba kuwa timu yake iko vizuri na itachukua ubingwa wa mashindano hayo mara baada ya kushika nafasi ya tatu katika awamu iliyopita huku akizitahadharisha timu nyengine zitakazofanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kujipanga vizuri kwani hawatakuwa na mzaha
‘.. Sisi tumejipanga kuchukua ubingwa na si kushiriki tu mashindano au tuwe wa kwanza au wa pili, Hapana lengo letu ni ubingwa, Yeyote atakaekuja mbele yetu ajipange ..’ Alisema
Aidha ameongeza kuwa Siri iliyowafanya wapate matokeo mazuri ni uwezo wa wachezaji wake katika kusikiliza maelekezo ya mwalimu na kuyafanyia kazi Kwa haraka
Nae goli kipa wa timu ya Shibula, Maila Makungu amewataka wachezaji wenzake kutobweteka na matokeo walioyapata leo huku akimshukuru mwalimu wa timu Kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kucheza sambamba na kuwaomba mashibiki nna wadau wa michezo kujitokeza kwaajili ya kuiunga mkono timu hiyo.
Kwa upande wake Kocha wa timu ya kata ya Buswelu Jofrey Mbarangu amefafanua kuwa wachezaji wake walipata fursa za kushinda mchezo huo kutokana na uzembe wameshindwa kufanya hivyo badala yake watajipanga upya katika msimu ujao waweze kufanya vizuri.
Akihitimisha Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Ndugu Kazungu Safari Idebe amewataka wananchi wa Jimbo la Ilemela kujitokeza katika mashindano hayo kwaajili ya kuziunga mkono timu zao sambamba na kuwataka wadau wa michezo na mawakala kutembelea viwanja vinapochezwa mechi mbalimbali kwaajili ya kuchagua wachezaji wazuri na kuwasajili katika timu zao
No comments:
Post a Comment