Friday, September 3, 2021

RAIS WA ZANZIBAR DK.MWINYI AKAGUA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA CHAKECHAKE PEMBA

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandisi Said Malik Said, akitowa maelezo ya michoro ya ramani ya ujenzi wa jengo jipya la Mama na Mtoto linalojengwa katika Hospitali ya Chakechake Pemba, akiwa katika ziara yake alipofika kukagua Mradi huo Kisiwani Pemba na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mattar Zahor Masoud na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar.Dkt. Fatma Haji Mrisho

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Daktari Dhamana wa Hospitali ya Chakechake Pemba Dkt.Abdulrahaman Said Mselemu, akitowa maelezo na changamoto zinazowakabili katika kazi zao, wakati wa ziara yake alipotembelea hospitali hiyo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Moa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

  

WANANCHI na Wafanyakazi wa Hospitali ya Chakechake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa ziara yake kutembelea ujenzi wa jengo jipya la Mama na Mtoto katika hospitali ya Chake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwananchi wa Chakechake Pemba Bw.Mohammed Haji akielezea kero yake, wakati wa ziara yake kutembelea Mradi wa Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Chakechake Pemba.na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi na Wafanyakazi wa Hospitali ya Chakechake Pemba katika viwanja vya hospitali hiyo, baada ya kumaliza kulikagua jengo la Mama na Mtoto linalojengwa katika eneo la hospitali hiyo,na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Mattar Zahor Masoud.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wa Chakechake Pemba baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Mama na Mtoto linalojengwa katika eneo la Hospitali ya Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu)  

No comments:

Post a Comment