Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) aliyevalia jezi ya timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) akizungumzana wachezaji wa timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) alipowatembelea wakiwa mazoezini katika viwanja vya Kidongo chekundu maarufu kama JK Park jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa akiteta na baadhi ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake (Twiga Stars na Tanzanite) alipowatembelea wakiwa mazoezini katika viwanja vya Kidongo chekundu maarufu kama JK Park jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika viwanja hivyo Waziri Bashungwa ameongea na wachezaji wa timu hiyo akiwalezea adhima ya serikali katika kuinua michezo nchini na kuwapongeza wanamichezo wote kwa kuzidi kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuibuka vinara katika michezo mbalimbali.
Waziri Bashungwa amesema timu za wanawake za mpira wa miguu kwa maana ya Tanzanite na Twiga Stars zimebeba jina la Tanzania na taifa linajivunia kwa kuwa na timu hizo, ambazo mara kadhaa zimeweka historia ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
“Sisi tutaendelea kuweka mazingira wezeshi ili muweze kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano mbalimbali, lakini hata huko mnako kwenda tembeeni kifua mbele mkijia kabisa Tanzania na watanzania wote wanawaamini na wako pamoja nanyi” alisema Waziri Bashungwa.
Kwa upande wake kocha wa timu za Taifa za wanawake Bakari Shime amemwelezea Waziri Bashungwa kuwa mashindano ya COSAFA yanayotarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini yatawasaidia kujiweka vizuri kwa ajili ya maandalizi ya kuwania kufuzu mashindano ya kombe la dunia mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment