Wednesday, August 18, 2021

KATIBA NA SHERIA WAANZA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA SITA

  

ADELADIUS MAKWEGA, WKS-DODOMA

Wizara ya Katiba na Sheria imetiliana saini na SUMA JKT katika ujenzi wake wa jengo la Ghorofa sita ambapo unatajiwa kuanza hivi punde na kukamilika ndani ya miezi nane kuanzia Agosti 18, 2021.

Akizungumza katika hafla fupi wizarani hapo Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome amesema kuwa zoezi hilo limeanza kama maagizo ya serikali na tayari fedha zimetengwa ili kuweza kufanyika ujenzi huo.

“Ninawakikishia Watanzania wote kuwa sasa  kazi inaanza baada ya taratibu zote kufanyika na uchaguzi wa SUMA JKT hauna shaka kwani tayari tushawapima katika ujenzi wa awali na kazi hii waliifanya vizuri sana.”

Katibu Mkuu Mchome aliongeza kuwa hata kama kuna changamoto za ujenzi  katika jengo letu la awali SUMA JKT wanazifahamu kuliko mkandarasi mwingine yeyote.

Tumepokea zaidi ya bilioni 22 kwa ujenzi wa awali na tunatarajia kama wakimaliza mapema kama tulivyokubaliana tutaingia katika awamu ya pili ya ujenzi wa jengo  la ghorofa tatu na watamalizia na awamu ya mwisho.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu ywa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Ali Shausi amesema kuwa anashukuriu Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuwapatia kazi hiyo, hilo linatoa ishara namna vyombo vya ulinzi na usalama vinavyofanya kazi kwa bidii, uadilifu na umakini.

“Hii ni Wizara ya nane sasa aabayo wameshatukabidhi kazi na ninatoa ahadi kuwa kazi hiyo itafanyika vizuri na kwa umakini mkubwa.”

Ni kweli kuna changamoto ya upatikanaji na baadhi ya vifaa vya ujenzi kama vile mchanga na kokoto kwa kuwa sasa wizara  nyingi na taasisi nyingi za Serikali zinajenga majengo yao lakini jeshi letu lina uwezo mkubwa wa kuwasiliana na wazabuni wote na tutapata vifaa vyote na kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa pia  na wakurugenzi kadhaa wa Wizara ya Katiba na Sheria akiwamo Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni Wizarani hapo Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) wa Jeshi Polisi ambaye ni pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uangalizi na Usimamizi wa Utajiri na Rasimali Asilia Bi Neema Mwanga akiambatana na wajumbe wake wote.

No comments:

Post a Comment