Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Tabora
WAZIRI wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amewaonya baadhi ya
viongozi wenye tabia ya kuingialia Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS)
huku akiwataka kuacha tabia hiyo mara moja.
Aidha, amesema ushirika sio idara ya serikali hivyo
hauwezi kuongozwa kama idara kwakuwa mamlaka yake ina mipaka na hakuna kiongozi
anayetakiwa kuingilia matumizi ya fedha wala kuzipangoa matumizi.
Waziri Mkenda ametoa agizo hilo (Jumamosi, Julai 3, 2021) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika
Kitaifa katika viwanja vya lipuli, Tabora, ambapo alisema kwa
kiasi kikubwa serikali imepambana kurejesha mali mbalimbali za ushirika
zilizokuwa zimeibiwa kupitia ushirika.
”Tumepambana sana na wabadhilifu kwenye ushirika na
kurejesha mali mbalimbali zilizoibiwa kupitia ushirika hivyo kurudisha imani ya
wanaushirika, na mali zao haziwezi kufanyiwa ubadhirifu wa aina yoyote.
Tutaendelea kusimamia ushirika kuhakikisha kwamba
unaendelezwa kwa weledi, uwajibikaji na uwazi ili watu wengi wakubali kujiunga
na ushirika kwa sababu unasaidia sana kunyanyua hali zao za kimaisha kwa kuwa ni
hiari kujiunga hakuna kulazimishwa,”alisema.
Alieleza kuwa ushirika ni hiari na msingi wa kwanza
duniani na kwamba ni kweli ushirika sio idara ya serikali hivyo hauwezi
kuongozwa kama IDARA YA SERIKALI KWAKUWA mamlaka yake kwenye ushirika yana
mipaka yake.
”Na hili ni muhimu kwa sababu kuna mahali ametokea
kiongozi mmoja kaingia kwenye AMCOS anatoa amri toa shilingi milioni ishirini
na tano hapa peleka kule, hatuna mamlaka hayo, ushirika ni hiyari ya
wanaushirika
”Na hapaswi kupelekesha wana ushirika wanapaswa kujisikia
kwamba ushirika ni mali yao, wasimame kidete, wasimamie shughuli zao bila
kuingiliwa kinyume na taratibu zinazokubalika,”alisema.
Alisisitiza anasema hilo kwa sababu kuanzia Waziri wa
kilimo (yeye), Mrajisi wa ushirika, wote lazima wajue mpaka upi wa kwao au si
wao
”Mpaka sasa tunakwenda vizuri ukiacha hilo tukio mtu
kwenda kutoa amri chukua hela za ushirika kutoka eneo moja kupeleka eneo ambalo
ushirika huo hauhusiki nalo kwenda kujenga shule,
”shule ni jambo zuri lakini hakuna mamlaka ya kiongozi
yoyote kwenda kuingia kwenye ushirika kuingilia fedha zao kuzipangia matumizi
hayo yatafanywa na wanaushirika wenyewe ,”alisema.
MWISHO
Thanks ni ujumbe mzuri wenye ufafanuzi maana tulipofikia sasa unasema ushirika ni mali ya serikali wananch tunaogopa kujiunga na kuendesha ushirika hauko huru utasikia mkuu wa mkoa au wilaya amefukuza bodi au watendaji bila kufuata utaratibu kila siku vyama hujikuta vikianza upya kila siku watendaji wapya hakuna MAENDELEO yoyote tanayoweza kuja kwa kubadili watendaji jioni na asubh tena anafukuzwa bila hata makosa
ReplyDelete