Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Profesa Siza Tumbo imewataka wataalamu wanaofanya tathimini ya uhakika wa usalama wa chakula na lishe kufanya tathmini hizo kwa kuzingatia mazingira husika kwa kuangalia mitazamo ya ndani ya nchi badala ya kutumia mifumo ya nje ambayo wakati mwingine hukosa uhalisia wa maisha ya watanzania. Profesa.
Profesa tumbo amesema hayo leo jijini dodoma wakati akizindua Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe Tanzania (MUCHALI) unaoratibiwa na Shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo.
Amesema hali ya kufanya tathmini nchini bado siyo sahihi kwani mara nyingi hutumika mbinu za Mataifa mengine katika kufanya tathmini za ndani ya nchi jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa marekebisho.
Pia amewahimiza watanzania kuzingatia ulaji wa vyakula vya asili vinavyojenga kinga na kuimarisha afyua badala ya kutumia vyakula vya kisasa ambavyo asilimia kubwa huchangia udhaifu wa kinga ya mwili kukabiliana na maradhi mbalimbali.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Lishe kutoka Shirika la Mpango wa Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO),Stella Kimambo amesema muongozo uliozinduliwa utatathmini hali ya chakula na lishe kwa ngazi ya mkoa na wilaya na kuanisha hatua muhimu ambazo zitakazochukuliwa na MUCHALI na wadau wengine wakati wa ukusanyaji, uchambuzi na usambazaji wa taarifa za usalama wa chakula.
No comments:
Post a Comment