Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akifungua maji katika moja ya vituo vya maji vinavyonufaika na mradi wa maji Munanila uliopo katika Kijiji cha Munanila Wilaya ya Buhigwe Mkoa wa Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akikagua Ujenzi wa Soko la la kisasa la Muyama Wilayani Buhigwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyarubanda aliposimama kuwasilimu akiwa njiani kuelekea wilayani Buhigwe. Makamu wa Rais yupo ziarani mkoani Kigoma. PICHA – OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Julai 17, 2021 amewatembelea na kuwasalimu wakazi wa Kijiji cha Kasumo kilichopo wilaya ya Buhigwe – Kigoma Mahali alipozaliwa.
Akiwa kijijini hapo Makamu wa Rais amewahakikishia wananchi wa eneo hilo kwamba serikali ya Awamu ya Sita itatekeleza mambo yote yaliopo katika ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 ilioahidi katika Wilaya ya Buhigwe na Mkoa wa Kiigoma kwa Ujumla.
Makamu wa Rais amewashukuru wananchi wa Kijiji hicho kwa hapo awali kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo la Buhigwe na baadae kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amewasisitiza wananchi wa Kasumo kuweka mkazo katika suala la elimu na kuhakikisha wale wote wanaostahili kusoma wanapata haki hiyo.
Makamu wa Rais anaendelea na ziara ya kikazi Mkoa wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment