Saturday, June 5, 2021

VIJANA WA KIJIJI CHA KIDAMALI WAMEWATAKA VIONGOZI KUJIBU MASWALI YA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO

Baadhi ya vijana  na wanawake wakipewa elimu kutoka mradi wa kuelimisha vijana na wanawake juu ya ushiriki wao katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC kwa ufadhili wa internews Tanzania 

Na Fredy Mgunda,Iringa. 

VIJANA na wanawake wa kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi mkoani Iringa wanakumbana na vikwanzo vya kupata elimu ya kufanya maamuzi kwenye mikutano ya serikali za mitaa na vijiji ili kuchangia shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Wakizungumza mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa kuelimisha vijana na wanawake juu ya ushiriki wao katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC kwa ufadhili wa internews Tanzania ambapo baadhi yao walieleza kutokuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Walisema kuwa kumekuwa na utekelezaji wa miradi mingi katika vijiji na mitaa yao ambayo ushirikishwaji wake umekuwa mdogo kiasi cha vijana wengi kutoshiriki kwa kiasi kikubwa.

Waliongeza kuwa kwenye mikutano ya hadhara mara kadhaa wamekuwa wakiuliza kuhusiana na jinsi miradi inavyotekelezwa lakini hawapati majibu yanayojitosheleza kiasi cha kuwakatisha tamaa vijana na wanawake kuuliza maswali ya mapato na matumizi. 

Vijana na wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu kutoka mradi wa kuelimisha vijana na wanawake juu ya ushiriki wao katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC kwa ufadhili wa internews Tanzania  ambapo baadhi yao walieleza  kutokuridhisha na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao jambo linalopelekea kuwa na mwamko mdogo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo.

vijana hao walisema kuwa ushiriki wa vijana na wanawake katika shughuli za maendeleo unapungua siku hadi siku, kutokana vijana wenyewe kutoona umuhimu wa kushiriki,kutopewa nafasi ya  kudadisi juu ya Miradi ya Maendeleo na kupewa majibu yasiyoridhisha.

Yeremia Kibasa na winfrida mgovano ni baadhi ya vijana katika Kijiji cha kidamali walisema wamekuwa wanakumbana na chuki pale ambapo wanaamua kuuliza maswali ya utekelezaji wa miradi ya kijiji au maswali yanayohusu suala zima la rushwa na ubadhirifu fedha katika miradi ya maendeleo. 

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Victor Simon alisema changamoto ya ushiriki wa vijana na wanawake katika shughuli za maendeleo hutokana na viongozi katika maeneo mengi kutofuatilia sera ya vijana na wanawake na kuwajulisha  namna  wanaweza kunufaika na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Naye mdau wa masuala ya maendeleo Mkoani Iringa Juma Makalla alisisitiza kwamba kutoshiriki katika shughuli za maendeleo kunapelekea vijana wengi kuwa tegemezi katika jamii na familia.

Mratibu wa mradi kutoka shirika lisilo la kiserikali la Iringa Development of Youth ,Disabled and children care {IDYDC} Ruben Magayane alisema kuwa mradi umejikita kuelimisha vijana na wanawake juu ya ushiriki katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji ili kuongeza hamasa kwa kundi la Vijana na wanawake kushiriki katika nyanja mbali mbali.

Magayane alisema kuwa vijana na wanawake wanatakiwa  kuwa mstari wa mbele kutumia fursa zilizopo ili kuhakikisha wanachangia katika shughuli za kimaendeleo za familia na jamiii inayowazunguka kwa kutoa maamuzi yenye faida chanya na wao sehemu ya wafanyaji maamuzi.

No comments:

Post a Comment