Saturday, June 5, 2021

MNEC SALIM ASAS : WANANCHI WA IRINGA FUATENI SHERIA NA KANUNI ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI


Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani nkoa wa Iringa MNEC Salim Abri Asas akibandika stika kwenye gari ikiwa ishara ya kuashiria kuwa uzinduzi umefunguliwa rasmiMkuu wa wilaya Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa angalia zoezi la ubandikaji stika kwenye gari ikiwa ishara ya kuashiria kuwa uzinduzi umefunguliwa rasmiMwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani nkoa wa Iringa MNEC Salim Abri Asas akiwa na Mkuu wa wilaya Richard Kasesela sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire pamoja na Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WANANCHI wa mkoa wa Iringa wametakiwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali mbalimbali ambazo zimekuwa na kuleta madhara kwa binadamu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni ya safari salama mkoani Iringa,mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani nkoa wa Iringa MNEC Salim Abri Asas alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kuzifuata sheria na kanuni za usalama wa barabrani ili kuepusha ajili barabarani.

Alisema kuwa imezuka tabia ya madereva wa vyombo vya moto kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi na kusababisha ajali huku wakiwa wanazitambua sheria hizo.

“Unakuta dereva anajua kabisa anavunja sheria za usalama barabarani lakini anaendelea kwa makusudi na kusababisha ajali,rai yangu kwa wananchi wote wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanafuata sheria hizo za usalama barabarani” alisema Asas

Alisema kuwa kumekuwa tabia ya matumizi mabaya ya zebra zilizopo mkoani Iringa kwa wananchi kuvuka katika eneo hilo huku anaongea na simu kuna madereva wa vyombo vya moto ambao nao hukiuka kwa makusudi sheria za barabarani.

MNEC Asas alisema kuwa imerudi tabia ya madereva bodaboda kupakia abiria zaidi ya mmoja (Mshikaki) jambo ambalo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani kwa kuwa inahatarisha usalama wa wananchi wanaotumia usafiri huo.

“Ukipakia mshikaki kunakuwa na hatari kubwa ya kupata ajali hivyo lazima madereva bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za msingi kwa kuhatarisha maisha ya binadamu” alisema MNEC Asas

MNEC Asas aliliomba jeshi la polisi kuendelea kusimamia vilivyo sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikipoteza maisha ya wananchi wengi bila sababu ya msingi hivyo jeshi la polisi linamamlaka zote za kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa vilivyo.

Alisema kuwa imezuka tabia ya madereva Bodaboda kuto vaa kofia ngumu kwa makusudi huku wakijua kuwa sheria ya usalama barabarani inakaza kwa lengo la kuwakinga na ajali ambazo zinazotea barabarani kwa kuokoa uhai wao.

Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada alisema kuwa usalama wa raia wa manispaa ya Iringa upo mikononi kwa wananchi wenyewe kwa kufuata sheria za usalama barabarani ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na jeshi la polisi mkoa wa Iringa.

Aliwataka wananchi wa manispaa ya Iringa kuhakikisha wanaulinda uhai wao wanapotumia vyombo vya moto ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika

Aidha meya Ngwada aliwaomba wananchi wa Manispaa ya Iringa kuendelea kufanya usafi katika maeneo ya makazi na maeneo ya biashara ili kuepusha kukumbwa na magonjwa ya milipuko ambayo inazuilika.

Ngwada aliwaomba wananchi wanaofanya shughuli za kibiashara pembezoni mwa barabara wanatakiwa kutafuta njia mbadala ya kujiepusha na ajali za barabarani kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuulinda uhai wao.

Ngwada alimalizia kwa kuwaambia wananchi wa manispaa ya Iringa kuwa wameanza kutafuta njia mbadala wa kutengeneza barabara zote ambazo zimeharibika kwa kuwa zimekuwa kero kwa watumiaji wa njia hizo.

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi wa kwanza hadi mwezi wa tano kumetokea ajali kumi na saba (17),vifo kumi na tano (15),watu waliofariki walikuwa wanaume tisa (9),wanawake sifuri (0) ajali za majeruhili zilikuwa mbili (2),watu waliojeruhiwa walikuwa wanaume kumi na moja(11) na wanawake watatu (3).

Alisema kuwa mwaka 2021 jumla ya ajali zilikuwa kumi na nne (14) pungufu kwa ajali tatu saw ana asilimia 18% ajali za vifo zilikuwa nane ambapo pungufu kwa asilimia 11%,waliofariki walikuwa wanaume nane na hakuna mwanamke hata mmoja,ajali za majeruhi zilikuwa sita nalilikuwa ongezeko la majeruhi wane na wanaume waliokuwa wamejeruhiwa walikuwa kumi na tano (15) na wanawake walikuwa tisa (9).

ACP Bwire aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uharifu na wahalifu na kuendelea kutii sheria bila shuruti ili kudumisha amani ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa aliwataka wakandarasi wanaopewa tenda ya kutengeza barabara kuhakikisha wanazingatia sehemu ya watembea kwa miguu ili kuepusha ajali ambazo sio za msingi.

Kasesela alisema kuwa barabara mpya zinazojengwa hivi sasa zinatakiwa kuzingatia watembeaji wa miguu,watu wenye ulemavu zinatakiwa kuwekewa alama ambazo zitawasaidia kuepusha ajali za barabarani.

Aliliagiza jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuhakikisha wanawakamata madereva bodaboda wote wanaoendesha chombo hicho huku wakiwa wamevaa ndali kwani ni kinyume cha sheria za usalama barabarani.

Kasesela ameugiza uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa kurekebisha barabara ya zizi ili kuepusha ajali na foleni ambayo huwa inatokea katika barabara hiyo na kuwataka jeshi la usalama barabarani kuwachukulia hatua kali wanaovunja sheria za usalama barabarani ili iwe onyo kwa wananchi wangine.

No comments:

Post a Comment