Tuesday, June 29, 2021

SHINYANGA MABINGWA MCHEZO WA KURUKA CHINI UMISSETA 2021

Mikoa ya Shinyanga na Pwani imeongoza kwenye mchezo wa kuruka chini katika Mashindano ya Taaluma na Michezo kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) kwenye fainali zilizofanyika leo Juni 29, 2021 katika uwanja A kwenye chuo cha walimu mjini Mtwara.

Msemaji wa UMISSETA 2021, John Mapepele amesema Musa Yusufu kutoka Shinyanga ameibuka kuwa mshindi wa kwanza baada ya kuruka umbali wa mita 6 na sentimita 71 akifuatiwa na Mpaji Gipson kutoka mkoa wa kigoma aliyeruka umbali wa mita 6 na sentimita 35 wakati nafasi ya tatu imechukuliwa na Alexander Jumanne kutoka Mkoa wa Geita aliyeruka umbali wa mita 6 na sentimita 34.

 Kwa upande wa wasichana Joha Mbaraka kutoka Mkoa wa Pwani ndiye Mshindi wa kwanza kwa kuruka mita 4 na sentimita 72 akifuatiwa na Witness Ibrahim kutoka Geita aliyeruka umbali wa mita 4 na sentimita 67 ambapo nafasi ya tatu ilichukuliwa na Diana Chacha kutoka Mara aliyeruka umbali wa mita 4 na sentimita 54.

No comments:

Post a Comment