Tuesday, June 8, 2021

DC KASESELA: AMEKANUSHA TUHUMA ZA KUMILIKI SHAMBA ISUPILO NA ENEO LA FAMILIA YA RODRICK MAHENGE

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifafanua namna gani ambavyo anazushiwa tuhuma za kumiliki shamba Isupilo na eneo la Rodrick Mahenge
Eneo la marehemu Rodrick Mahenge ambalo pia linamgogoro baina ya familia hiyo na wapagaki wa eneo hilo
Eneo la marehemu Rodrick Mahenge ambalo pia linamgogoro baina ya familia hiyo na wapagaki wa eneo hilo


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa wilaya ya Iringa amekanusha tuhuma za kuchangia mgogoro wa wananchi wa kijiji cha Isupilo na muwekezaji kampuni ya Overland mgogoro wa familia ya marehemu Rodrick Mahenge na wapangaji wake wanaogomea kulipa kodi ya pango waliopanga katika eneo la familia hiyo lilolopo Ipogolo Manispaa ya Iringa.

Akizungumza na viongozi wa kijiji cha Isupilo, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa tuhuma zinazoenezwa na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isupilo kuwa anachochea mgogoro huo sio za kweli.

Alisema kuwa kumekuwa na taarifa zinazosema kuwa anashamba la kufugia mifugo aina ya mbuzi katika shamba hilo lenye mgogoro baina ya wananchi na muwekezaji wa kampuni ya Overland.

Kasesela alisema kuwa alienda katika kijiji hicho kwa lengo la kutatua mgogoro huo ulikuwa umemfikia mezani kwake kama kiongozi na sio kumpendelea mtu yeyote yule.

Alisema kuwa shamba la muwekezaji kampuni ya Overland linahekari 1262 huku hekari 953 hazina mgogoro wowote na hekari 296 ndio zinamgogoro ambao kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha tuhuma hizo.

“Mimi sifugi mbuzi wa sina shamba katika kijiji cha Isupilo nashangaa tu natuhumiwa na baadhi ya wananchi kuwa namiliki shamba na kufuga mbuzi kitu ambacho ni uongo mkubwa amboa mimi naukataa kabisa” alisema Kasesela

Kasesela alimalizia kwa kusema kuwa lengo lake ni kuhakikisha anatatua mgogoro huo kwa amani ili kila mmoja apate haki zake bila kumpendelea mtu yeyote yule.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Isupilo Joachim Kisinini alisema kuwa mgogoro upo kati ya baadhi ya wananchi na muwekezaji na sio kweli kuwa mkuu wa wilaya ya Iringa anachochea mgogoro huo kwa manufaa yake.

Alisema kuwa shamba hilo lina hati ya mwaka 1929 na lilikuwa linamilikiwa na Rashid Kivike kwa kipindi hicho chote hadi pale alipoamua kuliuza kwa kampuni ya Overland na ndipo mgogoro ulipoibuka baina ya muwekezaji huyo na wananchi ambao wanaishi na kufanya shughuli za kilimo katika shamba hilo.

Kisinini alisema kuwa eneo la hekari 296 ndio linamgogoro baina ya wananchi na muwekezaji na ndio mkuu wa wilaya ya Iringa yupo kwenye mpango wa kuhakikisha anatatua mgogoro huo.

Aidha Kisinini alimalizia kwa kusema kuwa uongozi wa kijiji hicho hawaitambui hati hiyo kutokana na mmiliki wa awali Rashid Kivike kutolalamika mahali popote pale wakati wananchi wengine wakiendelea kufanya shuguli za kimaendeleo katika shamba hilo.

Alisema hadi hivi sasa muwekezaji anatumia hekeri 953 kwa shughuli zake na hizo nyingine hazitumii kwa kuwa zinatumiwa na wananchi licha kuwa bado kunamgogoro.

Katika mgogoro mwingine mkuu wa wilaya amekanusha kuhusu katika mgogoro wa familia ya Marehemu Rodrick Mahenge na wapangaji wake kwa kutengeneza tuhuma kuwa amejigawia eneo kwenye eneo hilo la familia hiyo.

Akizungumza na wasimamizi wa mirathi, Kasesela alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha anatatua mgogoro huo kwa amani na kuwaamuru wapangaji wote wanatakiwa kulipa kodi kwa wakati na wasipolipa wanatakiwa kuondolewa haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake Jeny mahenge alisema kuwa kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya familia na baadhi ya wapangaji ambao wamekuwa wanagoma kulipa kodi toka mwaka 2017 hadi hivi sasa.

Alisema kuwa familia imekuwa hainufaiki na chochote kile kutokana kutolipwa kwa kodi na wapangaji hao kukaidi kulipa kodi hizo.

Lakini pia alikanusha kuwa mkuu wa wilaya Iringa Richard kasesela hana eneo analomiliki katika eneo hilo la marehemu Rodrick Mahenge kama inayosemwa huko mitandaoni na mitaani na watu wasiojua chochote kile.

No comments:

Post a Comment