Thursday, May 27, 2021

WIZARA YA KILIMO YAANZA UTEKELEZAJI WA HOTUBA YA BAJETI

Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Wazalishaji wa Mbegu (TASTA) Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 27 Mei 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya mbegu Tanzania wakiwa katika majadiliano.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Wazalishaji wa Mbegu (TASTA) Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 27 Mei 2021. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Chimagu.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe maalumu kutoka Shirika la Chakula (WFP) Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 27 Mei 2021.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akimsikiliza kwa makini Muwakilishi Mkazi wa WFP Bi Sarah Gordon Gibson wakati alipokutana na kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 27 Mei 2021. 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi Mkazi wa WFP Bi Sarah Gordon Gibson Ofisini kwake Jijini Dodoma tarehe 27 Mei 2021. 

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Wizara ya Kilimo imeanza utekelezaji wa hotuba yake iliyowasilishwa bungeni tarehe 24/25 Mei 2021 ikiwa na mtazamo chanya wa kuimarisha masoko na tija katika mazao.


Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda tarehe 27 Mei 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe maalumu kutoka Shirika la Chakula (WFP) Ofisini kwake Jijini Dodoma.


Katika mkutano huo WFP imemuhakikishia Waziri wa Kilimo kuwa Shirika hilo litaendeleza ushirikiano maradufu baina yake na serikali ya Tanzania.


Akizungumza na Muwakilishi Mkazi wa WFP Bi Sarah Gordon Gibson amesema kuwa WFP imejipanga kuanza utekelezaji wa Miradi miwili kwa ajili kuwajengea uwezo wakulima wadogo katika mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora na simiyu ikiwa ni njia mojawapo ya mkakati wa kuongeza tija.


Pamoja na mambo mengine Waziri Mkenda ameiomba WFP pamoja na mazao waliyokusudia katika utekelezaji wake pia waongeze na zao la alizeti katika mkakati huo ili kuimarisha soko la mafuta nchini.


Kadhalika, katika kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora nchini Waziri Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Wazalishaji wa Mbegu (TASTA) ili kuainisha changamoto zinazoikabili sekta hiyo.


Waziri Mkenda ameagiza watendaji wa Wizara ya Kilimo pamoja na TASTA kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya mbegu nchini.


Katika hotuba aliyoitoa Waziri Mkenda Bungeni Jijini Dodoma aliainisha kuwa serikali imejipanga Kufanya utafiti wa mbegu bora zenye tija.


Katika hatua nyingine ujumbe huo maalumu kutoka Shirika la Chakula (WFP) ukiongozwa na Muwakilishi Mkazi wa WFP Bi Sarah Gordon Gibson umekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe.


MWISHO

No comments:

Post a Comment