Umoja wa wanawake Tanzania Mkoa wa Kagera katika kuadhimisha miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamefanya mambo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba ikiwemo kupatiwa elimu ya afya kuhusu salatani ya mlango wa kizazi pamoja na lishe bora.
Warsha hiyo imefanyika kaika viwanja vya kituo cha afya Zamuzamu kilichopo kata ya Bilele feburuari 01,mwaka huu, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wa mkoa na wilaya huku mgeni rasmi akiwa ni katibu mwenezi wa chama hicho Ndg. Hamimu Mahamudu.
Akitoa elimu kwa wanawake waliohudhuria warsha hiyo kuhusu salatani ya mlango wa kizazi Bi Dunia ameeleza kuwa watu walio hatalini kuambukizwa au kupata ugonjwa huu ni wasichana walioanza kufanya ngono kwa umri mdogo, mwanamke mwenye wanaume wengi kwa wakati mmoja, mwanamke anayevuta sigara na mwanamke mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Dunia ameongeza kuwa salatani hiyo inatibika hivyo wanawake wanatakiwa kujenga tabia ya kupima mara kwa mara kwa kuwa dalili zake hazionekani haraka japo madhara yake ni makubwa pale inapochelewa kutibiwa.
Kwaupande wake mtaalamu wa lishe kwaniaba ya afisa lishe manispaa ya bukoba amesema kuwa watoto wengi wamekuwa wakizaliwa wakiwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya udumavu, lishe duni kutokana na mama zao kutozingatia mlo kamili.
Ameonngeza kuwa tatizo la udumavu na lishe duni kwa watoto limekuwa sugu hasa kwa ukandaa huu wa Kagera hali inayopelekea kuwepo kwa namba kubwa ya watoto wenye udumavu na kuwashauri wanawake kuzingatia aina za vyakula wanavyotakiwa kula wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ili kumjengea mtoto afya njema.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo katibu mwenezi wa ccm Kagera Hamimu Mahamudu ameishukuru jumuiya hiyo kwa kuadhimisha kuzaliwa kwa chama chama chao kwa kuwapa wanawake elimu hasa inayo husu afya ya mama na motto maana kundi hilo ndilo linalotegemewa.
Amewataka wanawake waliopata elimu hiyo kuwa mabalozi wema kwa wanawake wengine kwa kuwapa elimu waliyoipata huku akiagiza vikao vyote vya chama hicho kwa ngazi zote kuweka agenda ya lishe.
“Ninakushukuru mwenyeki wa UWT kwa jambo hili, huwezi kuwaongoza wanachama au wananchi wakiwa hawana afya, kwa mantiki hiyo kama msemaji wa chama wa Mkoa huu naagiza kwenye vikao vyenu na vya chama kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa kuwepo na agenda ya lishe” Amesema Mahamudu.
Hamimu ameupongeza uongozi wa kituo cha afya Zamuzamu kwa usimamizi mzuri ambao umepelekea kituo hicho kuboreshwa na kuwa na wodi kubwa ya wazazi, chumba cha upasuaji, maabara ya kisasa na miundombinu iliyoimara huku kikiongeza idadi ya wattumishi kutoka watumishi 28 hadi 51 waliopo sasa.
Bi Anna Kajuna ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Bukoba mjini ambaye ameeleza mambo waliyoyafanya kituoni hapo ikiwemo elimu ya afya, upimaji wa salatani ya mlango wa kizazi, utoaji wa damu na ukaguzi wa miundombinu ya kituo hicho.
Mama Kajuna amewataka wanawake kuzingatia elimu waliyopata huku akiwataka kujenga tabia ya kupima afya hali itakayowapelekea kuzitambua afya zao pamoja na kuanza matibabu maramoja pale watakapogundulika na magonjwa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment