Tuesday, January 19, 2021

MEYA NGWADA AMPONGEZA SALIM ABRI ASAS KUCHANGIA MADAWATI 500

Mkurugenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) aliyetoa madawati 500 kwa halmashauri ya manispaa ya Iringa.

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imempongeza mkurugenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas kwa kuchangia madawati 500 kwa shule zenye uhitaji hasa kwa shule madarasa mapya kwa ajili ya wanafunzi wapya.

Akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Iringa,Meya wa Manispaa ya lringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa mkurungenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas amejitolea madawati 500 katika Shule mpya zenye uhaba wa madawati zilizojengwa na Manispaa kwaajili ya wanafunzi wapya waliochanguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari hayo.

Aliongeza kwa kusema kuwa mkurugenzi huyo wa kampuni ya Asas amekuwa anajitoa sana kwenye kuchangia shughuli za maendeleo manispaa ya Iringa kwenye sekta zote hivyo huyu ni mdau mkubwa wa maendeleo katika manispaa ya Iringa.

"Naomba kuchua nafasi hii kumpongeza ndugu Salim Abri Asas kwa juhudi zake ambazo amekuwa akichangia katika maendeleo katika maeneo ambayo wanahitaji msaada bila hata kuwa kumuomba yeye anajitolea tu"alisema Ngwada

Ngwada alisema kuwa madawati 500 ni mengi na yatasaidia kupunguza uhaba wa madawati katika shule zilizopo manispaa ya Iringa hivyo mkurugenzi wa kampuni ya Asas ameipinguzia mzigo halmashauri na wananchi wa madawati.

Katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alishukuru juhudi zinazofanywa na mkurugenzi wa kampuni ya Asas ambaye ni mjumbe wa halmashauri mkuu ya taifa ya chama cha mapinduzi kwa kazi anazozifanya za kimaendeleo mkoani Iringa kwa ujumla.

Hapi alimtaka afisa elimu kukaa na wakuu wa Shule za binafsi na za serikali ili kupunguza adha ya wanafunzi kubeba mabegi yenye uzito mkubwa pamoja na kupata muda wa kujisomea  masomo ya ziada.

Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa walimshukuru mkurugenzi wa kampuni ya Asas Salim Abri Asas kwa msaada huo wa madawati ambao utawapunguzia mzigo wazazi na serikali wa kutengenza madawati hayo.

"Madawati 500 mengi sana kwa halmashauri yetu ya manispaa ya Iringa hivyo kujitolea kwake kutasaidia sana wanafunzi wetu kusoma wakiwa kwenye madawati na mungu ambariki sana alipopunguza"walisema wananchi.

No comments:

Post a Comment