Kaimu Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu kusitishwa kwa mafunzo ya kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 wakati wa mkutano uliofanyika makao makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino mkoani Dodoma leo Januari 19, 2021, Mafunzo hayo yalipangwa kuanza hivi karibuni katika makambi mbalimbali ya JKT.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Kaimu Mkuu wa
Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Kanali Hassan Mabena wakati
akieleza kuhusu kusitishwa kwa mafunzo
ya kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 yaliyokuwa yaanze hivi karibuni
katika makambi mbalimbali hapa nchini hadi yatakapotangazwa tena.
Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) limesitisha kwa muda Mafunzo kwa kundi la kujitolea kwa mwaka 2020/2021 kwa
vijana waliokuwa wamechaguliwa kushiriki
mafunzo hayo yaliyotarajiwa kuanza hivi karibuni nchini kote.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu
Mkuu wa Utawala, Kanali Hassan Mabena wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo wilayani Chamwino
mkoani Dodoma.
“Kutokana
na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT inawataka
vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya
kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujitolea warejee majumbani kwao” alisisitiza
Kanali Mabena.
Pamoja
na hayo, Kanali Mabena amewataka vijana
ambao walikuwa hahawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi
waliyopangiwa mpaka watakapotangaziwa tena.
Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa likiwajengea vijana uwezo wa kujiajiri kupitia stadi za maisha wanazopata katika mafunzo yanayotolewa kwa mujibu wa sheria na yale ya vijana kujitolea, hivyo kuwawezesha kuwa wazalendo wanaoshiriki kikamilifu katika ujenzi waTaifa.
No comments:
Post a Comment