Sunday, December 6, 2020

SHULE YA KAKANGAGA YATAMBA KUENDELEA KUFANYA VIZURI,WAZAZI WAOMBWA KUWA WALEZI BORA KWA WANANFUNZI WAWAPO LIKIZO

Wahitimu wa kidato cha nne shule ya kiislamu ya sekondari Kakangaga wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati  wa mahafali ya 9, kabla ya kuingia ukumbini.

Mkuu  wa shule ya kiislamu ya sekondari Kakangaga Sheikhe Abdul-jalilu Sheikhe Siraji Mustapha akielezea masuala mbalimbali  ya shule kwa wazazi,wanafunzi  na wageni waalikwa wakati  wa mahafali ya 9 ya shule hiyo.

Wakati shule katika Maeneo mbalimbali hapa nchini zikianza likizo ya mwaka wa masomo 2020-2021 wazazi na walezi wamehusiwa kuwakaribu sana na watoto wao katika kipindi hicho Cha Mapumziko.

 

Imebainika kuwa wakati wa likizo wazazi huwapa uhuru uliopitiliza watoto wao bila kujua kuwa wanawaharibia na kuwapotezea kumbukumbu za masomo kwa kuwapangia kazi nyingi, kuwapa simu huku muda wa kujisomea ukiwa haupo kabisa.

 

Akisoma taarifa ya shule kwenye mahafali ya 9 ya shule ya upili Kakangaga Muslim Sekondari iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma, yaliyofanyika Desemba 05, mwaka huu, makamu mkuu wa shule hiyo Mwalimu Fahad Zaidi amesema kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto ya wanafunzi wanapotoka likizo kuwa wamebadirika kitabia na mienendo.

 

Ameeleza kuwa changamoto hiyo ni moja ya changamoto mbaya Sana amabayo huweza kuwarudisha wanafunzi nyuma kitaaluma licha wanakuwa wametoka shuleni wakiwa sawa.

 

Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa shule ya Kakangaga imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani yake ya kuanzia ngazi ya wilaya Hadi Taifa kwa kuongeza ufahulu Kila mwaka na kuufanya mkoa wa Kigoma kusomeka katika Ramani ya kusimama kielimu.

 

Kwaupande wake mkuu wa shule hiyo Sheikhe Abduljalilu Siraji ameushukuru uongozi wa wilaya ngazi ya wilaya na mkoa kw akuendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuitambua shule hiyo kwa kutoa mchango mkubwa wa elimu maana imebeba taswira ya mkoa wa Kigoma.

 

Amesema shule hiyo imekuwa ikibeba jukumu kubwa la kuwalea watoto katika maadili mema na kuwafanya kuwa kio katika jamii kwa kuwapa elimu ya dini na elimu sekula Hali inayowapelekea wanafunzi waliopita shuleni hapo kufanikiwa kwenye masomo yao ya juu pamoja na jamii inayowazunguka kuwaamini.

 

Ameongeza kuwa shule hiyo inayomilikiwa na Baraza kuu la waislamu Tanznaia (BAKWATA) ikisimamiwa na uongozi wa shule ya kiislamu ya Katoro iliyopo wilayani Bukoba mkoani Kagera inakumbwa na changamoto za vyumba vya madarasa baada ya kuongezaka kwa wanafunzi kutokana na shule hiyo kufanya vizuri pamoja na uzio kwaajili ya usalama wa wanafunzi na Mali za shule.

 

Mhe. Atashasta Nditiye mbunge wa Jimbo la Muhambwe na naibu waziri mstaafu wa wizara ya uchenzi na uchukuzi na mawasiliano, alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ambapo katika hotuba yake ameushukuru uongozi wa shule kwa kuendelea kuitangaza wilaya ya Kibondo kielimu  pamoja na mkoa wa Kigoma kwaujumla.

 

Nditiye amesema kuwa katika kipindi chake Cha miaka mitano iliyopita alikuwa akitoa ushirikiano mkubwa na shule hiyo na kutatua baadhi ya KERO zilizokuwa zikiwasumbua ikiwemo kero ya umeme.

 

Ameongeza kuwa ataendelea kushirikiana na shule hiyo pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wamiliki wa shule huku akiahidi January mwakani kukabidhi mifuko 100 ya Saruji kwaajili ya ujenzi unaonedelea wa vyumba vitatu vya madarasa na kutafuta namna nzuri ya kujenga uzio wa shule hiyo.

 

Aidha amewataka wazazi ppamoja na walezi kutoa ushirikiano mkubwa kwa walimu kwaajili ya malezi na makuzi ya watoto wao, na kuwatakia kuwa wanafatilia mienendo ya watoto wao na kutowaachia jukumu Hilo walimu pekeyao.

No comments:

Post a Comment