Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelezo ya ufafanuzi muda mchache baada ya ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini, 05 Desemba 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere - Dar es Salaam.
Kongamano hilo lililenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini amabayo ni moja kati shughuli zilizopangwa kufanyika katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020
Prof. Shemdoe ametolea ufafanuzi wa utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa wakati akifungua Maonesho hayo ya kutumia maeneo ya uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere mara kwa mara si tu kwa maonesho ya sabasaba ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Aidha, Prof. Shemdoe ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuweka maandalizi ya kuandaa maonyesho angalau kila roro mwaka ili watu wapate fursa za kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao ambazo zinazalishwa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment