Miongoni mwa madiwani hao pia yumo Mbunge wa Makete Festo Sanga ambao kwa kauli moja wamesema hawawezi kuipitisha taarifa hiyo kwani kuna baadhi ya miradi wanaitilia shaka hasa katika matumizi yake ya fedha ikilinganishwa na uhalisia wa miradi husika.
Wamesema,lazima wapate muda wa kuipitia taarifa hiyo kifungu kwa kifungu ili wajiridhishe kama fedha zilizotumika ni sawa na miradi inayoonekana kwenye taarifa hiyo.
Mgomo huo umetokea leo katika kikao cha kwanza cha baraza la madiwani tangu ufanyike uchaguzi Mkuu ambapo baada ya kula kiapo ndipo wakapewa ripoti hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waipokee na na kupitisha .
Kwa mujibu wa madiwani hao,kutokana na Mwongozo uliotolewa na Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI ) wanapaswa wapatiwe taarifa kabla ya siku saba ili waisome vizuri na kujiridhisha katika kazi ambazo zimefanyika.
Akizungumza katika kikao hicho Sanga amesema kuwa serikali imetoa mwongozo kwamba diwani anatakiwa apate taarifa siku saba kabla ya kikao ili kumwezesha kupata muda wa kusoma na kujiridhisha kama yale yaliyomo kwenye taarifa husika yana uhalisia.
Ameshauri kikao hicho kiahirishwe na badalanyake kifanyike kesho ili leo wajumbe wakaipitie taarifa hiyo na kisha wafanye maamuzi sahihi ya kuipitisha ama kutoipitisha taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Francis Chaula amepokea ushauri huo na kuahitisha kikao hicho hadi kesho.
No comments:
Post a Comment