Wazee wa wilaya ya Ilemela wametakiwa kukemea mmomonyoko wa maadili na vitendo visivyofaa katika jamii ili kujenga jamii iliyosawa na yenye maendeleo.
Rai hiyo imetolewa na mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wazee wa jimbo hilo kuwashukuru kwa mchango wao katika kukisaidia chama cha mapinduzi kupata ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi oktoba mwaka huu ambapo katika wilaya hiyo chama hicho kilishinda kwa asilimia 91 kwa nafasi ya Rais, asilimia 84 kwa nafasi ya ubunge na udiwani kwa kata zote 19 ikiwemo na madiwani wa viti maalum ambapo akawataka wazee hao kuchukua hatua katika kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili vinavyofanywa na vijana hasa kupitia mgongo wa siasa ikiwemo kuichafua nchi na kuihujumu ndani ya mipaka na nje ya mipaka ya nchi
‘.. Tukikaa kimya watoto wetu wataharibika, Lazima tuchukue nafasi yetu katika kuonya, kukosoa, Zamani ilikuwa ukikosea mzee yeyote anakuonya anakuchapa au kukusema bila kujali wewe ni mtoto wake wa kuzaa au la ..’ Alisema
Aidha Dkt Mabula akawataka wazee hao kuendelea kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanaleta maendeleo ndani ya jimbo hilo na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya ya Ilemela shekh Mohamed Yusuph mbali na kuishukuru serikali kwa hatua mbalimbali inazozichukua katika kuboresha maslahi ya wazee nchini ikiwemo utoaji wa huduma bure za afya, kuwalinda dhidi ya mauaji ya vikongwe na msamaha kwa baadhi ya kodi, Akamhakikishia mbunge huyo kuendelea kuchukua hatua dhidi ya kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa vijana
Nae Mzee Rashid Mvumbo kutoka kata ya Meco mbali na kumpongeza mbunge huyo kwa ushindi akaihakikishia serikali ushirikiano katika kuleta maendeleo sanjari na kuahidi kusisitiza wazee wengine kwa ngazi ya jamii kuchukua hatua dhidi ya mmomonyoko wa maadili katika familia zao pamoja na kutanguliza uzalendo kwa nchi.
No comments:
Post a Comment