Wananchi wa Njiapanda Kitongoji Midaho Kijiji Kikoma wakicheza na kufurahia ujio wa mbunge wao Mhe. Eng. Ezra John Chiwelesa katika maeneo yao na kuwaletea msaada wa vifaa vya ujenzi.
Wananchi wa wilaya Biharamulo Mkoani Kagera wamefurahishwa na kasi ya utekelzaji wa baadhi ya ahadi za mbunge wao alizozitoa wakati wa kipindi cha kampeini za uchaguzi mkuu 2020 hali iliyoanza kuwajengea matumaini makubwa kwa serikali awamu ya tano.
Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Biharamulo Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa ya kutembelea kata zote za jimbo hilo iliyoanza novemba 24,2020 kuhitimishwa leo tarehe 28 Novemba, mwaka huu, wananchi hao wamesema kuwa katika kipindi kirefu wamekuwa wakiwachagua wabunge lakini hawakuwahi kuwaona wakirudi kuwasikiiza.
Wamesema kuwa kitendo cha mbunge huyo kurejea jimboni na kuanza kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi tena kwa kipindi kifupi baada ya kuapa kimewagusa sana na kuanza kuamini kuwa changamoto sugu zilizowasibu kwa kipindi kirefu sasa zitaanza kutatuliwa na kuwafanya kuishi maisha safi.
Frances Mihanda ni afisa mtendaji kata Nyamigogo ambaye amesema kuwa katika kipindi chake cha utumishi katika kata hiyo zaidi ya miaka 7 sasa hakuwahi kumuona mbunge wa jimbo akija kwenye kijiji chochote kwaajili ya kuongea na wananchi hata kuwashukuru tu kwa kumchagua suala lililokuwa ikiwakatisha wananchi tama huku kero zilizopo kwenye kata hiyo kama visima vya maji, huduma za barabara na miundombinu nyingine zikiendelea kuwatesa wananchi.
Mwenyekiti wa kijiji Kikoma kata Rusahunga Deusi Kagusu amesema kuwa kijiji chake kimekuwa kikikabiliwa na tatizo la shule kutokana na ukubwa wa kijiji hicho hali inayowapelekea watoto wengine kushindwa kusoma kwasababu ya shule kuwa mbbali na makazi yao hivyo kuwalazimu kutembea umbali wa kilomita 30 kuifata shule.
Kigusa amesema kuwa ujio wa mbunge huyo kwenye kijiji hicho akiwa amewapelekea vifaa vya ujenzi ambavyo ni Saruji mifuko 20, Nondo 26 na Misumari kwaajili ya kuunga mkono jitihada za wananchi wa eneo la Njiapanda Kitongoji Midaho walioanza kujenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya mwalimu ikiwa ni kutaka kutoa elimu kwa watoto wao.
Kwaupande wake mbunge wa jimbo hilo amewataka wananchi kuendelea kuiamini serikali na kutoa ushirikiano ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao kwa urahisi huku akisistiza kuwa utaratibu huo utakuwa wa kudumu katika kipindi chake cha ubunge.
Ezra amesema kuwa ziara yake katika kipindi hiki ilikuwa kwaajili ya kutekeleza ahadi alizozitoa wakati akiomba ridha ya kuwa mbunge baada ya kuzunguka jimbo zima na kujionea mwenyewe hali halisi na maisha wanayoishi wananchi pamoja na mahitajio ya wananchi wengine.
Amesema kuwa wakati wa kampeini kila alipokuwa akipita vijana wengi walikuwa wakimwambia suala la michezo na kuomba kuwaletea mipira ambapo ameona kwa takribani kata zote 17 vijana wanauhitaji wa mipira.
“Kama tunnavyojua sasa tunaanza kutekeleza Ilani ya chama chetu, na mimi katika kampeini zangu niliahidi kulitimiza hilo kwanza na sasa nimeleta mipira kwa vijiji vyote 79 vya wilaya ya Biharamulo pamoja na mipira kwaajili ya shule zote za sekondari ili kuwawezesha vijana kuwa pamoja lakini kufanya mazoezi ili pale ligi ya EZRA BIHARAMULO CUP itakapoanza basi vijana wawe wamefanya mazoezi.” Amesema Eng.Ezra.
Ezra akiwa katika kitongoji cha Midaho sehemu ya Njiapanda alipoenda kukabidhi vifaa vya ujenzi alivyoviahidi amesema kuwa changamoto ya elimu katika kitongoji hicho ni kubwa kwa wananfunzi kutokana na shule kuwa mbali hivyo jitihada za wananchi kuanzisha ujenzi zimemshawishi kuwasaidia ambapo ameongeza kuwa wakifikia hatua ya kuezeka yeye ataleta pia mabati ili shule hiyo iezekwe.
Sanjali na hayo mbunge huyo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Biharamulo mjini wenye lengo la kuwaambia wananchi mikakati yake na vipaumbele vyake huku akieleza kuanzisha huduma ya gari la kubeba wagonjwa na mili ya marehemu jimboni humo bure.
No comments:
Post a Comment