Mkuu wa Uhusiano wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akieleza kwa waandishi wa habari athari za vipodozi vyenye viambata sumu vilivyoteketezwa na TBS mwishoni mwa wiki, Vipodozi hivyo vina thamani zaidi ya Shilingi Milioni 125.
Zoezi la uteketezaji wa vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani zaidi ya shilingi milioni 125 likiendelea mwishoni mwa wiki, Zoezi hilo limeteketezwa na TBS Jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora kutoka
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw. Gervas Kaisi akieleza hatua
zinazochukuliwa na Shirika hilo katika kudhibiti bidhaa zenye viambata sumu .
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza
vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani ya Shilingi milioni 125 baada
ya kufanyika kwa ukaguzi wa kushitukiza
kwenye maghala ya kuhifadhia vipodozi ambayo hayajasajiliwa.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa
mwishoni mwa wiki na TBS, Vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku vilikutwa katika
maghala la kampuni ya Kimario Cosmetics
hivi karibuni na wakaguzi wa TBS
Jijinii Arusha na kukamatwa kwa
mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009 pamoja na Marekebisho yake ya
Mwaka 2019.
“Mmiliki wa ghala hilo Pamphil L. Kimario
amelipa shilingi milioni 3.5 ikiwa ni gharama ya kuteketeza bidhaa hizo
hatarishi kwa afya ya binadamu
kwani zinapotumiwa huweza kusababisha
madhara mbambali kwa mtumiaji”,Inasisitiza taarifa hiyo
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Baadhi wa Watanzania
wamekuwa wakitumia vipodozi hivyo vyenye viambata vya sumu ambavyo vina
kemikali ya Mercury na Hydoroquinone kwa lengo la kung’arisha ngozi zao
na hata kubadili rangi ya ngozi hizo bila kujali madhara yatokanayo na
bidhaa hizo.
Vipodozi vyenye kemikali ya Mercury kwa Mujibu
ripoti ya Shirika la Afya Duniani(WHO) ya mwaka 2020, vikitumika kwa muda mrefu
vinasababisha magonjwa ya figo, mapafu, ngozi, macho mfumo wa fahamu mfumo wa
mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kinga ya mwili na kwa upande wa matumizi ya
vipodozi vyenye kemikali ya hydroquinone husababisha magonjwa ya kansa ya
ngozi.
Aidha, Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sheria ya
Fedha Na. 8 ya mwaka 2019 iliipa Mamlaka
TBS ya kusimamia usajili wa bidhaa za
chakula ,vipodozi , maghala ya kuhifadhia chakula na vipodozi pamoja na
migahawa na mahoteli jukumu lillilokuwa
likifanywa hapo awali na iliyokuwa Mamlaka ya Dawa Chakula na Vipodozi (TFDA).
Utekelezaji wa Sheria hiyo ya Fedha ulianza
rasmi tangu Julai 2019, hivyo kuwalazimu wauzaji wazalishaji na wauzaji wa vipodozi kusajili bidhaa hizo
pamoja na maghala ya kuhifadhia.
Shirika pia limeteketeza bidhaa nyingine
zisizofaa za vipodozi na vyakula zilizokamatwa
katika kaguzi zilizofanyika nyakati tofauti
katika maeneo mengine Arusha na nje ya Arusha katika kipindi cha Januari hadi
Novemba 2020.
TBS inaendelea na ukaguzi huu nchi nzima pamoja na kuwahimiza wazalishaji na wauzaji wa vipodozi kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zilizopo kwa kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala ili kuepuka usumbufu. Pia wauzaji wa vipodozi wanahimizwa kuwa na orodha ya bidhaa za vipodozi visivyoruhusiwa ambayo inapatikana katika tovuti ya Shirika www.tbs.go.tz
No comments:
Post a Comment