Mgeni Rasmi wa mashindano ya NBC Dodoma Marathon ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake wakati wa kuhitimisha mashindano hayo yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma na kushirikisha wanariadha kutoka hapa nchini na nchi za Kenya, Malawi na Uganda ambapo washiriki elfu 3000 wameshiri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan akitunuku medali kwa mshindi wa kwanza wa mbio hizo kwa kundi la washiriki wa kilomita 42 baada ya kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya NBC Marathan yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini Dodoma Dodoma na kushirikisha wanariadha kutoka hapa nchini na nchi za Kenya, Malawi na Uganda ambapo washiriki elfu 3000 wameshiriki.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan akishiriki mbio za NBC Dodoma
Marathon zilizofanyika leo Novemba 22,
2020 Jijini Dodoma na kushirikisha
wanariadha kutoka hapa nchini na nchi za
Kenya, Malawi na Uganda ambapo
washiriki elfu 3000 wameshiriki.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan
amewataka wanawake nchini kujitokeza kupima afya zao mapema ili kujua hali zao
hatua inayosaidia kupambana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi.
Mama
Samia amesema akiongea wanamichezo walioshiriki mbio za Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC) Dodoma Marathon yaliyofanyika leo Novemba 22, 2020 Jijini
Dodoma.
“Akinamama
mjitokeze kupima afya zenu mapema, msiogope kwenda kupima saratani ya mlango wa
kizazi hatua inayosaidia kupambana na saratani hii na kulinda afya za watu
wetu” amesema Mama Samia.
Katika
mashindano hayo, Makamu wa Rais Mama Samia amewapongeza wanawake kwa kujitokeza
kwa wingi kwenye mbio hizo hatua
inayoonesha ni mwanzo mzuri wa kupambana na saratani ya shingo ya kizazi
nchini.
Aidha,
Makamu wa Rais Mama Samia amesema mashindano ya NBC Dodoma Marathon yamekuja
muda mwafaka hatua inayosaidia wanamichezo kujiandaa vema katika mashindano ya Olimpik
yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni 2021 Tokyo nchini Japan pamoja na
kuchangisha kiasi cha takriban zaidi ya Sh. milioni 75 ambazo zimeelekezwa
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Jijini Dar kusaidia mapano dhidi ya saratani
ya shingo ya kizazi.
Katika
hatua nyingine Makamu wa Rais Mama Samia amesema kuwa Serikali ipo mstari wa
mbele katika kukuza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kama alivyoahidi Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
kufungua Bunge la 12 hivi karibuni Jijini Dodoma.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.
Hassan Abbasi amesema wizara yake imesimama kidete kuhakikisha sekta ya michezo
nchini inasonga mbele ambapo kwa mara ya kwanza imetenga fedha kwenye bajeti ya
mwaka 2020/2021 kwa ajili ya kusaidia timu za taifa katika mashindano ya
kimataifa.
Dkt. Abbasi amemhakikishia Makamu wa Rais Mama
Samia kuwa sekta ya michezo hawatamuangusha katika mambo yote yanayohusu
michezo mbalimbali ambapo atafanya pia ziara katika mashirikisho yote ya
michezo na vyama vya michezo nchini ili kuhakikisha Serikali na wadau wa
michezo wanakuwa na kauli moja ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.
Naye
Mkurugezi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt. Julius Mwaisalege
amehakikishia Makamu wa Rais Mama Samia kuwa fedha zilizopatikana kutokana na
usajili wa wanariadha wa mbio za NBC Dodoma Marathon zitatumiwa na kufanyiwa
kazi iliyokusudiwa ili kuokoa maisha ya wanawake nchini.
Dkt. Mwaisalege amesema fedha hizo zinalenga
kutoa elimu ya ugonjwa wa saratani, kufungua vituo 25 na kuandaa wataalamu 100
watakaosaidia wananchi kupima saratani ya mara kwa mara hatua itakayosaidia
kuepukana na ugonjwa huo na wakigundulliwa kuwa nao waweze kutibiwa mapema na
kupona ili waendelee na shughuli zao za kimaendeleo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Bw. Theobald Sabi amesema kuwa
benki hiyo wameona ni vema mapato yote yanayotokana na usajili wa wanariadha
zielekezwe kwenye vita na mapambano kwa ugonjwa wa saratani ya shingo ya
kizazi.
Bw.
Sabi ameongeza kuwa njia zote
zinazotumika kwenye mbio za NBC Dodoma marathon zimepimwa na mtaalamu kutoka
Shirikisho la Riadha Duniani Oktoba 17, 2020 na kutunukiwa vyeti vya utambuzi
na uthibitisho na vipo tayari Dodoma.
Fauka
ya hayo, Bw. Sabi amesema benki hiyo imepanga kuendelea kuwa wadhamini wa mbio
hizo kwa miaka mitano mfululizo ambazo zinatarajiwa kuwa na mvuto kitaifa,
kikanda na kimataifa zinazoshirikisha mbio za kilomita 5, kilomita 10, kilomita
21 na kilomita 42.
Mbio hizo za NBC Marathon zimehusisha wanariadha 3000 wakijumuisha wanariadha kutoka hapa nchini, 19 kutoka nchini Kenya, 12 kutoka Uganda pamoja na wanariadha wanne (04) kutoka Malawi.
No comments:
Post a Comment