Kiasi cha shilingi milioni 95 kitatumika kukarabati miundombinu ya elimu ya shule ya sekondari Shibula na shule ya msingi Igogwe kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo ya shule hizo katika kata ya Shibula ili kuwa na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia.
Hayo yamebainishwa na mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Ilemela Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa kata hiyo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Ilalila Senta ambapo amewataka wananchi hao kuchagua wagombea wa chama chake kwani wanathamini na kutambua umuhimu wa elimu na wamekuwa wakichukua jitihada mbalimbali za kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule mpya tatu za msingi, tatu za sekondari na mbili za kidato cha tano na sita ili kuwarahisishia Watoto upatikanaji wa elimu na kuwaepusha na kujiingiza katika vitendo ovu vyenye kukatisha ndoto zao
‘.. Katika sekta ya elimu tumetenga milioni 95 kwa shule za Igogwe na Shibula ndani ya kata yenu ili zikajenge miundombinu ya vyoo, hatutaki watoto wetu wakapate tabu ..’ Alisema
Aidha mgombea huyo akaongeza kuwa zaidi ya bilioni 10 zimetolewa na Serikali ya Dkt John Magufuli kwaajili ya upatikanaji wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari zinazotumiwa na wananchi wa wilaya ya Ilemela huku akihamasisha vijana wa wilaya hiyo kutumia fursa za kujikwamua kiuchumi zinazoletwa na Serikali ya awamu ya tano kutokana na miradi inayoendelea kutekelezwa ikiwemo mikopo inayotoka manispaa, mradi wa stendi ya kisasa ya mabasi na malori Nyamhongolo na ujenzi wa meli ndani ya Ziwa Viktoria.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake mkoa wa Mwanza (UWT) Bi Hellen Bogohe akawataka wanawake wa kata hiyo kuhakikisha wanachagua wagombea wa CCM kwa nafasi zote tatu ili ikawe rahisi kupata maendeleo huku akiwasisitiza kutumia njia zote kushawishi makundi mengine kukipigia kura chama cvha mapinduzi
Nae mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha akawataka wananchi hao kukiamini chama chake badala ya kujaribu wagombea kutoka vyama pinzani ambao hawana Ilani wala uwezo wa kutatua kero zao.
No comments:
Post a Comment