Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili
kulia) akiwa katika ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza chokaa cha
Neelkanth cha jijini Tanga kukagua utekelezaji wa sheria ya mazingira.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima
akiangalia mojawapo ya mawe yanayotumika kutengenezea chokaa katika kiwanda cha
Neelkanth cha jijini Tanga ambacho kinalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo
kufikiwa na vumbi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili
kulia) akiwa katika ziara ya kutembelea kiwanda cha kutemgeneza chokaa cha
Neelkanth cha jijini Tanga kukagua utekelezaji wa sheria ya mazingira.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima
amemuelekeza mwekezaji wa kiwanda cha chokaa cha Neelkanth Chemical cha jijini
Tanga kubuni njia mbadala ya kuzuia vumbi kutoka na kusambaa hewani hivyo
kuleta athari kwa wananchi.
Sima alitoa
agizo hilo jana alipofanya ziara ya kukagua kiwanda hicho ambapo pamoja na
mambo mengine ililenga kumpa maelekezo ya namna ya kuendesha shughuli bila
kuathiri mazingira.
Alibainisha
kuwa mashine zilizopo hapo hazina uwezo wa kuzuia vumbi kusambaa jambo ambalo
ni hatari kwa afya ya wafanyakazi na wananchi wakati moshi unapofuka
hewani.
Alilielekeza
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wapime na waangalie
ni madhara gani ya kiafya kwani unakwenda kwenye makazi ya watu.
“Mazingira
ya kiwandani hapa ni ya kawaida lakini tunashuhudia moshi na vumbi vikisambaa
ni sawa wana consultant (mshauri)
hapa standards (viwango) zinatofautiana hivyo ndio maana nimeelekeza NEMC
wapime washauri nini kifanyike,” alisema.
Aidha,
Naibu Waziri Sima alisisitiza kuwa pamoja na Serikali kualika wadau kuwekeza
katika sekta ya viwanda lakini pia inao wajibu wa kuhakikisha viwanda vinafanya
shughuli zake bila kuathiri mazingira na wananchi wanaozunguka.
Kwa upande
wake Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Ndimbumi Yoram alisema kumekuwepo
na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu vumbi na moshi vinatoka kiwandani
hapo.
Alitoa
mwito kwa mwekezaji huyo ambaye pamoja na kujikagua na kutoa ripoti kwa Baraza
hilo lakini pia awaruhusu kufanya ukaguzi wakati mashine zinafanya kazi ili
waweze kushauri.
“Tunaona
vumbi kwenye ambalo limetokana na kusaga mawe haya ya kutengenezea chokaa
lakini kwa sababu mitambo imezimwa hatuwezi kujua linatoka wapi hivyo mwenye
kiwanda awe muwazi aturuhusu tukague kikiwa kinafanya kazi ili tujue vumbi
linatoka wapi na tuweze kumshauri,” alisema Ndimbumi.
Nae
Mkurugenzi wa kiwanda hicho Rashid Hamoud aliishukuru Serikali kupitia kwa
Naibu Waziri huyo kwa kutembelea na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa.
No comments:
Post a Comment