Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi na Wadau wa Utatu wa sekta ya Kazi na Ajira wa Nchi Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuelekea Mkutano wa Mawaziri wa sekta hiyo utakaofunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Machi 5, 2020 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji mwenye dhamana ya Utangamano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo.
Wawakilishi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia ajenda zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwakilishi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akichangia hoja wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu wa sekta ya Kazi na Ajira wa SADC ikiwa ni hatua za kuelekea katika Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Sekta ya Ajira na Kazi wa SADC, utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (kulia), akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwakilishi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. (Wa pili kutoka kulia) ni Naibu Katibu Mtendaji mwenye dhamana ya Utangamano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo, Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii na Rasilimali Watu SADC Bi. Duduzile Simelane naMwakilishi wa Sekretarieti ya SADC, Bw. Maxwell Parakokwa.
Mwakilishi kutoka Zambia akichangia mada wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu, Maafisa Waandamizi na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment