Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wanawake wajasiriamali mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Wanawake Wajasiriamali kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea chimbuko la Siku ya Wanawake Duniani katika ufunguzi wa maonesho ya wanawake wajasiriamali mkoani Simiyi kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akieleza jitihada za mkoa katika kuhakikisha wanawake wanawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wakati wa ufunguzi wa maonesho ya wanawake wajasiriamali mkoani Simiyi kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya washiriki wa Msafara wa Kijinsia kutokomeza ukatili ilioanzia mkoani Latavi na kupoita katika mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iirnga, Tabora, Shinyanga na kumalizikia katika Wilaya za Maswa na Bariadi mkoani SImiyu wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akiupokea Msafara huo mkoani Simiyu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa atazitaja Halmashauri ambazo hazitatoa mikopo kwa wanawake kwa aslimia 50 ya mapato yake kuwa adui wa maendeleo ya wanawake.
Waziri Ummy ameyasema hayo mkoani Simiyu wakati akifungua maonesho ya wanawake wajasiriamali na kupokea msafara wa kijinsia wa Twende Pamoja uliomalizikia mkoani humo.
Waziri Ummy amesema kuwa suala la kutenga fedha kwa ajili ya mikopo ya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu sio suala la hiari bali lazima kwani lipo kisheria.
"Kabla ya tarehe 30 June tutazitaja Halmashauri zote ambazo hazikutoa mikopo kwa wanawake kwa asilimia 50 na tutazitaja kama maadui wa maendeleo ya wanawake" alisema
Ameongeza kuwa wanawake wakiwezesha watachangi kwa silimia kubwa ukuaji wa uchumi kwani kwa takwimu zilizopo asilimia 60 ya chakula kinazaliswa na wanawake na Serikali inaendelea kuhakikisha wanawake wanawezehswa kiuchumi.
“Tutahakikisha wanawake wanawezeshwa kiuchumi kwani tumepitisha Sheria ya utoaji mikopo bila riba kwa wanawake ili kuwawezesha kupata mikopo itakayowasaidia kuinua biashara zao” alisema
Aidha Waziri Ummy mawataka wamamchi kutofumbia macho vitendo vya ukatili vinavyotolea katika maneno yao na hasa wananume kujitokeza kutoa taarifa kwani vitendo hivi hawafanyiwi wanawake pekee bali hata wanaume wanafanyiwa vitendo vya kikatili.
“Niwatake wanawake kutokuwa sababu ya kufanyiwa vitendo vya kikatili kwani kuna wanawake wamekuwa akiona vitendo vya kikatili kuwa suala la kawaida ” alisema
“Natoa mfano kuna utafiti umefanyika na kubaini katika wanawake waliulizwa swali kuwa kama ikitokea ukauunguza mboga je ukipigwa na mumeo kwa kitendo hiko ni wanawake asilimia 20 walijibu ni sawa lakini sio sawa kabisa” alisema
Akizumgumza kuhusu chimbuko la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amaeema wananwake walikuwa ahawapati nafasi stahiki katika jamii ukilinganisgawa na wanaume hivyo Umoja wa Miatfa uliona ni jambo sahihi kuwa na Siku maalum ya kukumbushana kuhusua masuala ya wanawake.
No comments:
Post a Comment