Mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Fredrica Shirima, akipimwa urefu na Mkaguzi wa Afya MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Saredho Hussein, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwa wamemmbeba mwenzao, kama mfano wa kumpa huduma ya kwanza mtu aliyepata ajali ya kuvunjika viungo, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakimsikiliza Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza (OSHA), Moteswa Meda, wakati akiwaelekeza mfano wa kumpa mtu huduma ya kwanza pindi anapopata dharura, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Kaimu Mtendaji Mkuu, MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda, ukitoa elimu kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA , yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu wa Waziri Mkuu Bw. Raymond Gowelle, akikabidhiwa cheti cha ukaguzi katika maeneo yote ya ofisi hiyo na Kaimu Mtendaji Mkuu MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda, kwenye zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA kuhusu usalama katika maeneo ya kazi, yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa, jijini Dodoma Februari 1, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAMLAKA ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imetoa cheti kwa Ofisi ya Binafsi ya Waziri Mkuu baada ya kufanyia ukaguzi katika maeneo yote ya ofisi hiyo na kuonesha kuwa yamekidhi viwango.
Cheti hicho kimetolewa jana jioni (Jumamosi, Februari 1, 2020) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda na kupokelewa na Katibu wa Waziri Mkuu Bw. Raymond Gowelle.
Akikabidhi cheti hicho, Bi Khadija aliipongeza Ofisi hiyo kwa kuonesha mfano wa uetekelezaji wa sheria, ambapo amezishauri ofisi nyingine za umma ziige.
“Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu imeonesha mfano wa kuigwa kwa utekelezaji wa sheria, kwani walituita tukaja kufanya ukaguzi na tukatoa maelekezo ya namna ya kuboresha baadhi ya maeneo na wamerekebisha.”
Alisema baada ya kutekeleza maelekezo hayo suala lililokuwa limebakia ni upimaji wa afya kwa wafanyakazi pamoja na kutoa mafunzo ya huduma ya kwanza ambayo yamefanyika leo (jana).
Mtendaji huo alisema ni muhimu kwa ofisi zote kuzingatia sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji wa afya na mafunzo ya OSHA, pia watumishi wa Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu walikumbushwa namna bora ya kufanyakazi kwa uadilifu. Mafunzo yalitolewa na watalaamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Watumishi hao waliushukuru uongozi wa ofisi kwa kuandaa zoezi la upimaji wa afya ambao ulikuwa na muitikio mkubwa, mafunzo ya huduma ya kwanza pamoja na kukumbushwa kuhusu uadilifu na matumizi ya madaraka na ofisi kwa manufaa ya umma.
No comments:
Post a Comment