Tuesday, February 18, 2020

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAPONGEZWA UANDAAJI BAJETI

Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Robert Mtengule akiongoza kikao cha mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini Ofisi ya Masajili wa Vyama vya Siasa, F. Mazone akizungumza wakati wa kikao cha mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma. Kulia ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Robert Mtengule.
Afisa Usimamizi wa Fedha(FMO) kutoka Wizara ya Fedha na Mipango,Bw. Ezekiel Odipo ambaye pia ni Msimamizi wa Dawati la Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa akichangia mada wakati wa kikao cha mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya Mwaka 2020/2021 toka ofisi hiyo wakifuatilia maoni ya Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje toka Wizara ya Fedha na MipangoBw. Robert Mtengule katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ORPP jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment