Monday, February 3, 2020

CCM NYAMAGANA YAKAGUA UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITAL YA SEKOU TOURE





Kuelekea miaka 43 ya kuzaliwa CCM, Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana aungana na Kamati ya Siasa ya Kata ya Isamilo kukagua ujenzinwa jengo la Mama na Mtoto katika hospitali ya Sekou Toure.

Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana ndugu Geofrey Kavenga ameongozana na wajumbe wa kamati ya siasa ya Kata ya Isamilo, pamoja na Katibu wa UVCCM Wilaya ndugu Malanyingi Matukuta katika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto lenye ghorofa 5 katika hospital ya Sekou Toure. 

Ujenzi huo ulioanza mwezi Juni, 2019 unategemea kukamilika Tarehe 30 Juni, 2020 litakuwa na uwezo wa kuchukua vitanda 270, chumba cha upasuaji, kliniki za mama na watoto.

Katibu wa CCM ndugu Geofrey Kavenga amempongeza mkandarasi kwa kuwa na kasi ya ujenzi na kumtaka akamilishe kwa wakati ili kupunguza msongamano katika wodi za zilizopo sasa.

Pia ndugu Kavenga amewapongeza madaktati na wauguzi kwa kutimiza wajibu wao vizuri na kupelekea kutokuwa na malalamiko toka kwa wagonjwa wanapata huduma za kitabibu katika hospitali hiyo.

Gharama za ujenzi huo ni fedha bilioni 10 na hadi sasa ujenzi umetumia kisasi cha fedha bilioni 4.

Maadhimisho ya miaka 43 ya CCM yanafanyika kwa kamati za siasa za matawi, kata, wilaya na mkoa kufanya ziara za ukaguzi wa miradi ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM na kilele cha sherehe hizi ni tarehe 8 February, 2020 kwa kufanyika mikutano ya ndani.

Chama Cha Mapinduzi kimeanza wiki la sherehe la kudhimisha miaka 43 toka kuzaliwa kwake mwaka 5 February, 1977 baada vyama vya TANU na ASP kuungana.

No comments:

Post a Comment