Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo January 21 amepokea Mchango wa Shehena ya Ndoo 500 za Rangi za nyumba kutoka Kampuni ya utengenezaji wa rangi za Billion Paint iliyomuunga mkono katika kuhakikisha madarasa ya wanafunzi Mkoani humo yanakuwa katika Mwonekano Mzuri na wakupendeza.
RC Makonda amesema Rangi hizo alizopatiwa zitatumika kupaka madarasa zaidi ya 381 yanayojengwa na Serikali kwaajili ya Wanafunzi 5,970 ambao walifaulu vizuri kwenda kidato cha kwanza lakini wakakabiliwa na changamoto ya uchache wa vyumba vya madarasa lakini kupitia uongozi thabiti wa serikali ya awamu ya tano madarasa hayo yapo hatua ya mwisho kukamilika na kukabidhiwa kabla ya March 28 mwaka huu.
Aidha RC Makonda amepongeza kiwanda hicho kwa kuamua kurudisha fadhila kwa wananchi kupitia mchango wa Rangi hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zitaenda kutatua changamoto mbalimbali kwenye miundombinu ya majengo ya wanafunzi.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema amefurahi kuona Kiwanda hicho kinamilikiwa na Kijana Mzawa alieamua kuitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza uchumi wa Viwanda na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 40 kiwandani hapo.
No comments:
Post a Comment