Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,akitia saini
kwa kutumia kifaa maalum,ikiwa ni kuridhia Makubaliano ya Sekta ya Nishati yaliyokubaliwa
katika Mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wapili
kulia) akichangia mada katika Mkutano wa Baraza na Mawaziri wa Afrika Mashariki
wakati wa majadiliano ya sekta ya Nishati kwa nchi wanachama.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili
kulia) na Kamshna Msaidizi wa Nishati Jadifu wa Wizara ya Nishati, Edward
Ishengoma( kwanza kulia) wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano wa Baraza la
Mawaziri wa Sekta ya Nishati katika nchi za Afrika Mashariki unaofanyika kwa
njia ya mtandao,ambapo hapa nchini ulifanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili
kushoto) na Watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizochini yake
wakifuatilia Majadiliano ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Sekta ya Nishati
katika nchi za Afrika Mashariki unaofanyika kwa njia ya mtandao,ambapo hapa
nchini ulifanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,
amesaini makubaliano ya Sekta ya Nishati ya mkutano wa Baraza na Mawaziri wa
Afrika Mashariki kwa niaba ya Waziri ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani.
Mkutano huo umefanyika Januari 14, 2019,
ambapo kila nchi huufanya nchini kwake, hapa nchini mkutano huo umefanyika
jijini Dodoma kwa kushirikisha Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati,
Mashirika pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo.
Majadiliano ya Mkutano huo huendeshwa kwa njia
ya mtandao (Video Conference) kwa kuwakutanisha Mawaziri wa sekta husika kutoka
nchi zote wanachama.
Mkutano huo hujadili taarifa mbalimbali
iliyowasilishwa kwao na Makatibu Wakuu wa Wizara husika katika sekta hiyo zinayohusu
miradi mbalimbali ya maendeleo ya Sekta ya Nishati katika nchi wanachama.
Taarifa hiyo ya Makatibu Wakuu,
iliyowasilishwa kwa Mawaziri hayo imezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Umeme, Nishati Jadidifu, Mafuta
pamoja Gesi.
Baada ya majadiliano hayo, Mawaziri wote wa Sekta
ya Nishati wa nchi wanachama wa wameridhia na kusaini makubaliano ya kisekta,
kwa lengo la utekelezaji.
Mawaziri walioshiriki mkutano huo ni kutoka
nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda pamoja na Burundi.
No comments:
Post a Comment