Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Watumishi wa sekta ya ardhi wa Halmashauri nne za mkoa wa Rukwa (Hawapo pichani) jana wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Rukwa. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Khalfan Haule na kushoto ni Kamishna Msaidzi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Thadei Kabonge.
Watumishi wa sekta ya ardhi katika Halmashauri nne za mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi mkoani Rukwa jana.
Na Munir
Shemweta, WANMM -RUKWA
Makusanyo ya kodi ya
pango la ardhi katika halmashauri za mkoa wa Rukwa yamemvuruga Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula baada ya kuelezwa kuwa
hadi kufikia Desemba 2019 jumla ya shilingi milioni 148.2 zilikusanywa na halmashauri
zote nne sawa na asilimia 7.9 .
Akiwa katika ziara
yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Rukwa jana
ambapo alikutana na watumishi wa sekta ya ardhi, Dkt Mabula alishangazwa na
namna maafisa ardhi wa halmashauri hizo wasivyofuatilia makusanyo ya kodi ya
pango la ardhi kiasi cha kuzifanya halmashauri hizo kukusanya kiasi kidogo cha
fedha.
Alisema, haiwezekani
ndani ya miezi sita halmashauri nne za mkoa wa Rukwa zikusanye asilimia 7.9 ya
kodi ya pango la ardhi jambo alilolieleza kuwa linatia mashaka kama halmashauri
hizo zitaweza kufikisha hata asilimia hamsini ya makusanyo ya kodi ya pango la
ardhi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2019/2020.
Kwa mujibu wa Taarifa ya
mkoa wa Rukwa iliyosomwa na Mrasimu Ramani wa mkoa wa Rukwa Kelvin Maungi,
katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri za mkoa huo
zilikadiriwa kukusanya jumla ya sh 1,880,000,000.00 ambapo Manispaa ya
Sumbawanga ilikusanya kiasi cha sh. 94,253,273.00, Halmashauri ya wilaya ya
Nkasi sh. 16,494,189.00, Kalambo sh 1,793,550.00 na Halmashauri ya wilaya ya
Sumbawanga sh 35,680,575.00 na hadi hadi Desemba 2019 jumla ya shilingi
148,221,587.00 zilikusanywa kwa halmashauri zote sawa na asilimia 7.9.
‘’Wakurugenzi wako busy
na masuala mengine, mkoa mzima una silimia 7.9 ya makusanyo ya kodi ya pango la
ardhi! ni aibu na hamuwezi kufikia asilimia 50 ya makusanyo naagiza wote
mkafanye uhakiki wa wadaiwa wa kodi ya ardhi na muwapelekee ilani ili
watakaokaidi wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi’’ alisema Dkt Mabula.
Aidha, Naibu Waziri
Mabula aliagiza kufikia Machi 2020 lazima kuwe na mabadiliko ya utendaji kazi
kwenye sekta ya ardhi kwa halmashauri za mkoa wa Rukwa, vinginevyo atafikiria
kama wakuu wa idara wanatosha kuendelea na nafasi zao na kusisitiza kama ni
Mkuu wa Idara au Afisa Ardhi Mteule ataondolewa.
Dkt Mabula alisema mikoa
yote aliyoitembelea kwenye ziara zake za kukagua utendaji kazi wa sekta ya
ardhi imefikisha asilimia thelathini ya makusanyo ya kodi ya ardhi lakini mkoa
wa Rukwa umemsononesha sana na kumuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda
Thadei Kabonge atoe maelezo kuhusiana na utendaji kazi wa Wakuu wa idara kama
wanafaa kushika nafasi zao.
Hata hivyo, Naibu Waziri
Mabula alibainisha kuwa kulingana na taarifa zilizokuwa kwenye mfumo wa
kielektronik Manispaa ya Sumbawanga ilitakuwa kukusanya Bilioni 6.7,
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga milioni 20, Kalambo milioni 1.6 na Nkasi
milioni 16 hiyo inatokana na halmashauri hizo kuwa na malimbikizo ya wadaiwa
kodi ya pango la ardhi.
---------------------------------------MWISHO----------------------------------------------
No comments:
Post a Comment