Friday, January 24, 2020

Kusainiwa kwa makubaliano kati ya Barrick na Twiga kuna faida nyingi - Waziri Bashungwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa kampuni ya Barrick Dkt. Mark Bristow katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kapuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 .Halfa iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Januari 24, 2020.

Na Mathias Canal, WazoHuru Blog

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameimulika dhamira njema ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika mtazamo wake wa kuimarisha Uchumi wa nchi.

Akizungumza na mtandao wa Wazo Huru Blog leo tarehe 24 Januari 2020 muda mchache baada ya kukamilika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya makubaliano ya kuendesha kwa pamoja kampuni ya Twiga ya uchimbaji wa Madini kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ambapo kwasasa kampuni mpya ya ubia ya Twiga, Waziri Bashungwa amesema kuwa itakuwa na utashi mkubwa katika kuimarisha Uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya madini.

Ameongeza kuwa Serikali itakuwa na hisa ya asilimia 16 jambo hilo ni muhimu kwa sekta ya madini kwani litaimarisha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na mafanikio makubwa ya kiuongozi na kiuchumi. 

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo muhimu kabisa kupitia ushirikiano huo  katika nchi itakuwa ni watanzania kupata haki ama stahiki yao wakiwa ndio wenye rasilimali hiyo.

Kadhalika, Waziri Bashungwa amasema kuwa makubaliano hayo yamefungua mlango wa mfano wa kuigwa kwenye bara la Afrika na Dunia kwa ujumla wake kuhusu usimamizi wa rasilimali kwa nchi zinazoendelea unavyopaswa kuendeshwa.

Katika mahojiano hayo na Waziri Bashungwa hakusita kumpongeza Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuonyesha dhamira yake ya kiuongozi katika usimamizi wa rasilimali za nchi na uongozi katika bara la Afrika.

Amesema kuwa, Rais Magufuli ameonyesha uthubutu, uwezo wa kiuongozi, na jinsi ya kuliongoza Taifa lenye rasilimali nyingi kama Tanzania kwani ameonyesha weledi katika usimamizi wa sekta ya madini kadhalika sekta zingine sio tu sekta ya madini kuwa ndio sekta kiongozi katika mauzo ya bidhaa kwenda nje ya nchi, bali makubaliano hayo sasa yanafungua fursa na muingiliano wa shughuli za kiuchumi zitakazofanyika chini ya kampuni mpya ya Twiga na biashara katika sekta nyingine za uzalishaji na huduma. 

MWISHO

No comments:

Post a Comment