Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo leo tarehe 24 Januari 2020 wakati wa siku ya pili ya kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara, bodi za mazao na taasisi kinacho tathamini utendaji kazi wa nusu mwaka kufikia Disemba 2019 Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara, bodi za mazao na taasisi kinacho tathamini utendaji kazi wa nusu mwaka kufikia Disemba 2019 Jijini Dodoma wakifatilia kwa makini amelekezo ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 24 Januari 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa siku ya pili ya kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara, bodi za mazao na taasisi kinacho tathamini utendaji kazi wa nusu mwaka kufikia Disemba 2019 Jijini Dodoma.
Na Revocatus Kassimba, Wizara ya
Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga
ameagiza wakurugenzi wakuu wa bodi za mazao chini ya wizara ya kilimo kutenga
fedha kwa ajili ya kufanya utafiti ili kuongeza tija ya uzalishaji.
Waziri Hasunga ametoa maelekezo hayo tarehe
24 Januari 2020 jijini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya kikao kazi cha
Menejimenti ya Wizara, bodi za mazao na taasisi kinacho tathamini utendaji kazi
wa nusu mwaka kufikia Disemba 2019.
“Bila kuwekeza fedha za kutosha kwenye
utafiti kilimo kitaendelea kukua kwa kasi ndogo, hivyo nawaagiza watendaji
wakuu wa bodi kuweka bajeti ya utafiti
mwaka 2020” alisema Waziri wa Kilimo
Katika kikao hicho wajumbe walionesha
kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya uzalishaji kwenye mazao ya kimkakati ya biashara
kama tumbaku, mkonge,kahawa, pareto na chai.
Akitoa taarifa ya hali utendaji
kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Tumbaku Stanley Mnozya alieleza katika mwaka 2019/20 jumla ya tani 70,087 zilinunuliwa zenye
thamani ya shilingi Bilioni 230.3
Mnozya aliongeza kusema licha ya zao
la tumbaku kuwa la pili kwa kuingiza mapato zaidi nchini linakabiliwa na changamoto
ya kukosekana kwa uhakika wa soko na uwezo kidogo wa wakulima kuzalisha
kutokana na mfumo wa kilimo mkataba kutoeleweka vizuri.
“Bodi
inaendelea na majaribio ya aina mpya nne za mbegu ya tumbaku ya mvuke
toka China ili kuongeza tija kwa mkulima “
alisema Mkurugenzi Mkuu huyo.
Kwa upande wa Bodi ya Kahawa taarifa
iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Prof Jamal Adam imeonyesha uzalishaji wa
kahawa kufikia Disemba 2019 ulifikia tani 55,979 kati ya lengo la tani 50,000.
Prof Jamal ametaja aina za kahawa
zilizouzwa kuwa ni Robusta tani 22,320 Arabika
laini (Mild Arabica) 32,057 na Arabika ngumu (Hard Arabica) tani 1,602 na kuingiza mapato yenye thamani ya Dola za kimarekani 87,527,779 mwaka 2019.
Alitaja sababu ya kufikia mafanikio
haya kuwa ni bei nzuri katika soko la dunia na kuongezeka kuwa ubora wa kahawa ya Tanzania
iliyokusanywa toka vyama vya ushirika.
Prof Jamal alitaja changamoto
inayoikabili bodi ya kahawa ni uzalishaji mdogo wa miche bora ya kahawa nchini, ambapo mwaka 2019
walizalisha miche milioni 3.6 kati ya lengo la kuzalisha miche milioni 8.
“Tutaendelea kushirikiana watafiti hususani
TARI kuwekeza katika utafiti wa miche ili kufikia lengo la Wizara kuongeza
wigo wa wakulima kupanda kahawa bora ” alisema Prof Jamal
Wakati huo huo Waziri wa Kilimo Japhet
Hasunga ameagiza watafiti wa madawa na viuatilifi nchini kutumia zao la pareto
kuzalisha viuatilifu bora kwa matumizi ya wakulima.
Hasunga alisema hayo kufuatia taarifa
iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pareto Lucas Ayo kusema Tanzania
inashika nafasi ya kwanza Afrika na ya pili duniani kwa uzalishaji wa pareto.
‘’Ni wakati sasa wataalamu kutumia pareto
kuzalisha madawa na viutilifu bora kwenye viwanda vya ndani ili kukidhi soko la
wakulima na kuepusha uwepo wa viuatiflifu visivyo na ubora”alisisitiza Hasunga
Taarifa hiyo ya Bodi ya Pareto
ilionesha kuwa hadi kufikia Desemba 2019 tani 1,627 kati ya lengo la tani 2,600
za pareto zilizalishwa nchini na kuliingiza taifa mapato ya shilingi Bilioni 4.28
kufikia Disemba 2019.
Akitoa mchango kuhusu umuhimu wa
utafiti, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Dkt Geofrey
Mkamilo alisema “ tupo tayari kushirikiana na bodi zote za mazao kufantya
tafiti zitakazokuja na suluhisho la tija ya mazao kuongezeka” hivyo akashauri
bodi za mazao kujipanga kifedha .
Takwimu za uzalishaji mazao nchini
zinaonesha kupungua kwa uzalishaji na ubora kwenye mazao ya biashara nchini hali
inayopelekea nchi kukosa mapato ya kutosha, hivyo kuhitaji utafiti.
Waziri wa Kilimo anaendelea na vikao
vya Menejimenti kupitia taarifa za utendaji kazi wa Bodi za Mazao na Taasisi
zote zilizo chini ya Wizara yake na kuweka malengo na mikakati ya kuimarisha
utendaji kazi kwa mwaka 2020/2021.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment