Tuesday, January 14, 2020

DKT. NDUGULILE AWAPIGA TAFU WANANCHI UJENZI WA SEKONDARI UTENGULE USONGWE MBALIZI


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kulia) akikabidhi mifuko 50 ya saruji kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kwa ajili ya kumalizia vyumba tisa vya madarasa katika jitihada za kuunga mkono nguvu za wananchi katika ujenzi wa madarasa hayo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akichanganya zege kwa ajili ya kupiga lipu katika Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kwa ajili ya kumalizia vyumba tisa vya madarasa katika jitihada za kuunga mkono nguvu za wananchi katika ujenzi wa madarasa hayo.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipiga lipu katika moja ya chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kwa ajili ya kumalizia vyumba tisa vya madarasa katika jitihada za kuunga mkono nguvu za wananchi katika ujenzi wa madarasa hayo.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa Kata ya Utengule Usongwe wakati wa zoezi la ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa katika hule hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia ramani ya jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kitengo cha Mama na Mtoto.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila mara baada ya kumtembelea ofisini kwake wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila na  baadhi ya watendaji  mkoa Ofisi ya rais TAMISEMI  na Wizara anayosimamia mara baada ya kuzunumza na Mkuu wa Moa huo wakati wa  ziara yake ya kikazi mkoani humo.


Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wananchi wa Mji wa Mbalizi mkoani Mbeya kujikita katika kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo mjini Mbalizi mkoani Mbeya alipokuwa akishiriki katika ujenzi wa vyumba tisa vya Madarasa ya Shule ya Sekondari Utengule Usongwe kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kuamsha ari ya wananchi katika kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuwaunga mkono pale wanapoanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao.

"Wizara hii inahusika na masuala yote ya maendeleo ya kazi yetu kubwa ni kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea na kushiriki katika shughuli za maendeleo" alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali ya Awamu ya tano inataka kuona wananchi wanafanya kazi wanajishugulisha na shughuli za mendeleo kwa kuchangia katika miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bw. Benedict Mahenge ameishukuru Serikali wananchi na wadau walijitolea katika kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo kwani itasaidia kupunguza adha ya wanafunzi kukaa wengi katika darasa moja.

Aidha Afisa Elimu Kata ya Utengule Usingwe George Mtawa amesema ujenzi wa vyumba vya madarasa tisa umekuja kutokana na kuwa na idadi kubwa ya shule za msingi na ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba hivyo wananchi waliamua kuanza ujenzi huo ili kuondokana na changamoto ya watoto kukosa madarasa ya kusomea.

Naye Diwani wa Kata ya Utengule Usongwe Elia Mkono amesema kuwa wananchi wa Kata hiyo wameamua kujenga vyumba vya madarasa hayo ili kuhakikisha watoto 981 wanapata madarasa ya kuanza kidato cha kwanza katika Shuke hiyo.




No comments:

Post a Comment