Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza matumizi ya zana za kilimo wakati akizungumza kwenye Kongamano la tatu la kilimo na mifugo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo mbele ya Ndg Ramadhan Majubwa ambaye ni Mratibu wa shamba la mfano la mafunzo ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwenye Kongamano la tatu la kilimo na mifugo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la mfano la mafunzo ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwenye Kongamano la tatu la kilimo na mifugo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza matumizi ya zana za kilimo wakati akizungumza kwenye Kongamano la tatu la kilimo na mifugo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Viuatilifu wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kwenye Kongamano la tatu la kilimo na mifugo lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro, jana tarehe 4 Disemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro
Serikali imesema kuwa imejipanga kuhakikisha kuwa inawawezesha wakulima
kuboresha sekta ya kilimo kupitia mpango kabambe uliobuniwa na serikali wa
kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili-ASDP II.
ASDP awamu ya pili imejikita katika kuboresha kilimo kuwa chenye tija ili
kuimarisha kipato cha wakulima nchini hivyo kupitia programu hiyo wakulima
watanufaika na mafunzo yatakayotolewa na wataalamu wa kilimo ikiwa ni pamoja na
matumizi sahihi ya zana bora za kilimo
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo jana tarehe 4
Disemba 2019 wakati akihutubia kwenye Kongamano la tatu la kilimo na mifugo lililofanyika
katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro.
Amesema kuwa
maendeleo ya kilimo katika nchi yoyote Duniani yanategemea teknolojia bora na za
kisasa kwani matokeo ya teknolojia duni ndio yaliyopelekea kukosekana kwa
kilimo bora.
Amesema kuwa Programu ya kuendeleza kilimo awamu ya pili ASDP II ina
malengo matatu mahususi ambayo ni pamoja na kuwa na usimamizi bora wa ardhi, Uongezaji
wa thamani wa mazao na Kuongeza tija na uzalishaji ili kuwa na matumizi sahihi
ya mbegu bora, Viuatilifu, Mbolea na zana bora za kilimo.
Waziri Hasunga, amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanalima
kilimo cha hasara badala ya kulima kilimo cha kibiashara chenye tija na
uzalishaji mkubwa hivyo programu hiyo itakuwa muarobaini wa maboresho ya sekta
ya kilimo.
Waziri Hasunga amekipongeza Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Mkoani
Morogoro kwa kutoa mafunzo ya teknolojia za kisasa kwa wakulima ambao kwa kiasi
kikubwa wakulima wameendelea kunufaika na mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment