Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao hicho cha
majumuisho ya ziara ya ujumbe wa Benki ya Dunia wa kufuatilia utekelezaji wa
Mradi wa ERPP kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara Kilimo, Jijini Dodoma
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao hicho cha
majumuisho ya ziara ya ujumbe wa Benki ya Dunia wa kufuatilia utekelezaji wa
Mradi wa ERPP pamoja na Wajuumbe wa mkutano huo
Kiongozi
Ujumbe wa Benki ya Dunia, uliokuwa ukiongozwa na Bwana Holger Kray, Mtaalam wa
Masula ya Kilimo cha Kimkakati katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini
pamoja na Bibi Sarah Simon Mwandamizi wa Masuala ya Kilimo Benki ya Dunia
Tanzania
Na Issa Sabuni-Wizara ya Kilimo, Dodoma
Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe ameonya wakandarasi watatu waliopewa
kazi ya kujenga miundombinu ya skimu za umwagiliaji katika mradi wa kuongeza
tija na uzalishaji zao la mpunga (ERPP) mkoani Morogoro kukamilisha kazi hiyo
ndani ya miezi mitatu ijayo.
Agizo hilo
amelitoa jana Tarehe 4 Disemba 2019 wakati wa kikao cha tathmini ya miradi ya
ukarabati wa skimu za umwagiliaji na maghala inayofadhiliwa na Benki ya Dunia na
kusimamiwa na wizara ya kilimo kilichofanyika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma.
“Ili
kuhakikisha miradi hii inakamilika ndani ya muda mfupi, naagiza mratibu wa
mradi huu January Kayumbe kutokwenda mapumziko mwisho wa mwaka hadi wakandarasi
hawa waliozembea wakamilishe miradi ifikiapo Aprili 2020” alisema Mhandisi
Mtigumwe.
Katibu Mkuu
huyo amemtaka Mratibu wa Mradi wa Kuongeza Tija na Uzalishaji wa zao la Mpunga
(Expanded Rice Production Project – ERPP) Mhandisi January Kayumbe kusimamia
kwa ukaribu wakandarasi ili miradi ikamilike na kuwa na ubora unaokusudiwa na
serikali.
Mhandisi Mtigumwe
ametaja wakandarasi ambao hawajakamilisha kazi kuwa ni Lukolo Construction
Company Ltd inayojenga miundombinu ya shamba la Mbegu la Msimba, lenye ukubwa
wa hekta 640, linalomilikiwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA).
Pili,
Kampuni ya Confits Company Ltd inayojenga miundombinu ya skimu ya umwagiliaji
Msola Ujamaa Wilaya ya Kilombelo ambaye amefanya kazi kwa asilimia 25, na tatu
Kampuni ya Goba Construction Ltd inayofanya kazi ya ujenzi wa miundombinu
katika skimu ya Kigugu Wilaya ya Mvomelo imefanya kazi kwa asilimia 29.
Katika
hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameelezea mafanikio yaliyofikiwa na mradi huo
tangu ulipoanza kuwa wakulima wa mpunga wamepata maarifa
ya kilimo cha kisasa cha mpunga kulikosaidia kuongeza tija na uzalishaji.
“Mavuno ya
mpunga yameongezeka kutoka tani 1.8 mwaka 2015/2016 na kufikia tani 5 hadi 6
kwa hekta mwaka 2018/2019 chini ya mradi wa ERPP “alisema Katibu Mkuu wizara ya
Kilimo.
Kwa upande
wake Mtaalam wa Masuala ya Kilimo cha Kimkakati katika Ukanda wa Afrika
Mashariki na Kusini mwa Afrika kutoka Benki ya Dunia Bwana Holger Kray ameiomba
Wizara kufanya ufuatiliaji wa karibu ili wakandarasi wa ujenzi skimu za
umwagiliaji wakamilishe miradi hiyo ili wakulima wanufaike kwa uzalishaji
kuongezeka pia kipato cha kaya na taifa.
Mradi wa
Kuongeza Tija na Uzalishaji wa zao la Mpunga (ERPP) ulianza kutekelezwa mwaka
2015/2016 ambapo fedha kiasi cha dola za Marekani Milioni 22.9 zilitengwa kwa
ajili ya utekelezaji upande wa Tanzania Bara na Visiwani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment