Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwasalimia wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)
Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiongea wa wachezaji wa timu ya IUO wakati wa mchezo katika yao dhidi ya Irole fc(PICHA KUTOKA MAKTABA)
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Asas Super League 2019/2020
hatua nane bora imemaliza hatua ya mzunguko wa tatu kwa timu ya mafinga academy
kuongoza kundi B na Isiman Fc kuongoza kundi A huku timu ya mafinga academy
wakiongoza kwa kufunga magoli kumi.
Kufuatia kutamatika kwa
mzunguko wa tatu wa Asas Super League 2019/2020 kundi Alinaongozwa na timu ya
Isimani fc yenye alama saba na magoli ya kufunga matano huku ikiwa imefungwa
goli moja tu katika michezo mitatu ya awali.
Kidamali fc na kalinga fc
wanalinga alama kwa kila timu kwa kuwa na alama nne huku wakitofautiana kwa
idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku Kidamali fc akiwa na magoli ya
kufunga matano na wamefungwa magoli mawili tu na timu ya kalinga wakiwa
wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli manne.
Timu ya Young Stars wakiwa
wanaburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa wana alama moja huku wakiwa wamefungwa
jumla ya magoli sita katika michezo mitatu waliyocheza katika mzunguko wa
kwanza wa Asas Super League 2019/2020
Kwa upande wa kundi B,timu ya
Mafinga Academy wanaongoza kundi B wakiwa wamekusanya jumla ya alama tisa huku
wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa wamefunga jumla ya magoli
kumi na kufungwa magoli mawili kwenye michezo mitatu ya awali ya kundi B.
Timu ya Mkimbizi fc,Nzihi fc na
Irole Fc zote zimekusanya jumla ya alama mbili kwenye michezo mitatu huku
wakiwa wametofautiana kwenye magoli ya kufunga na kufungwa,ukiangalia Mkimbizi
Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa magoli matatu,Nzihi fc wamefunga magoli
mawili na kufungwa magoli manne na Irole Fc wamefunga magoli mawili na kufungwa
magoli saba na ndio timu inayongoza kwa kufungwa magoli mengi kuliko timu
yeyote ile kwenye hatua ya nane bora.
Asas Super League 2019/2020
itaendelea siku ya ijumaa tarehe sita mwenzi wa kumi na mbili kati Kidamali Fc
na Isimani fc mchezo utachezwa katika uwanja wa Kidamali na ikumbukwe kuwa
kwenye nmchezo wa awali timu ya Isimani ilishinda kwa goli moja bila.
No comments:
Post a Comment