Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika maeneo
hayo wakiwa kwenye eneo la tukio siku ya tarehe 1/10/2019
walipofukiwa.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri wa
Madini Stanslaus Nyongo wa katikati meza kuu, kushoto kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, kulia ni Katibu
mkuu wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na Yuma yake ni
Kamishna wa Madini Mhandisi David Mlabwa.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoa tamko la serikali la
kusitishwa kwa zoezi la uokoaji.
********************************
Na Issa Mtuwa “WM” – Geita
Majonzi na huzuni vimetawala kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo wa
Imalanguza wilaya ya Geita kata ya Lwamgasa katika Kijiji cha Imalanguzu,
mara baada ya kuwasili Naibu Waziri wa Madini Stanslausi Nyongo
mgodini hapo akiwa na viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya
Madini, uongozi wa mkoa na viongozi wa dini kwa ajili ya kwenda kusitisha
shughuli za uokoaji wa wachimbaji wadogo wawili Karos Msukuma Paulo
mwenyeji wa Chato na Kulwa Joseph Mahungija mwenyeji wa Busolwa
Nyang’wale waliofukiwa kifusi siku ya tarehe 1/10/2019.
Usitishaji wa zoezi hilo umefanyika tarehe 9/11/2019 ikiwa ni siku 39 tangu
wachimbaji hao wafukiwe na kifusi kutokana na uwepo wa changamoto
mbalimbali zilizo jitokeza katika kipindi chote cha uokoaji.
Ripoti maalam ya
timu ya wataalam wa uokoji imeeleza kuwa kumekuwa na changamoto
nyingi wakati wote wa ukoji zilizopelekea kuwa na ugumu wa kuwaokoa
wachimbaji hao.
Akiwasilisha taarifa ya wataalam wa uokoaji iliyoishauri serikali kusitisha
kwa zoezi hilo la uokoaji kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,
mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga amemwambia Naibu Waziri
wa Madini kuwa miongoni mwa changamoto zilizojitokeza wakati wa
uokoaji ni pamoja na uwepo wa maji chini ya mgodi, mwingiano wa
magogo mbalimbali chini ya shimo la mgodi, na kutokuwa na usalama
katika eneo hilo hata kwa vyombo vya uokoaji.
Maganga aliongeza kuwa, kulikuwa na wataalam wa makundi mbalimbali
ya uokoaji na vifaa vya kutosha kutoka kwa jeshi na uokoaji, mgodi wa
dhahabu wa Geita (GGM), na makampuni mengine kutoka kwenye migodi
mbalimbali, lakini pamoja na juhudi zote hizo imeshindikana kupatikana
kwao.
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa siku ya tukio hilo, kwenye shimo hilo
kulikuwa na wachimbaji 5 ambapo 3 kati yao waliokolewa siku hiyo hiyo na
wawili hawakuweza kupatikana hadi zoezi hilo la uokoaji linasitishwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri Nyongo, akiongea kwa masikitiko na
majozi kwenye hadhara hiyo, Nyongo amesema kwanza lililotokea ni bahati
mbaya na kwamba serikali imesikitishwa na tukio hilo na kwamba iko
pamoja wafiwa na wachimbaji wote.
Ameongeza kuwa, serikali inathamini sana hata uhai wa mtu mmoja kuliko
dhahabu au madini yote yaliko chini na ndio maana inasisitiza wachimbaji
kuchimba kwa kufuata utaratibu na sharia ili wachimbe kwa kuzingaatia
usalama ili kuepukana na majanga kama hayo.
Nyongo ametowa kauli ya serikali ya kuhitimisha shughuli za uokoaji na
kutoa maelekezo kuhusu eneo hilo ambalo wachimbaji hao wamefukiwa na
kifusi.
“Na sasa tunakwenda kufanya ibada ya kwenda kuwazika wenzetu, viongi
wetu wa dini wako hapa watatuongoza katika ibada hiyo kwa ajili ya
maombi. Natamka kuwa, shughuli zote za uchimbaji katika eneo ambalo
tunaamini kuwa ndipo wezentu hawa wapo, basi eneo hilo litambuliwe
rasmi kuwa ndio kabuli lao na kama kuna undelezaji wa shughuli ya
uchimbaji utaendelea katika eneo lingine na kwa utaratibu mwingine.”
alisema Nyongo.
Nyongo pia alitoa maagizo kwa afisa madini mkazi mkoa wa Geita na timu
yake kusimamia usitishwaji wa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo
mpaka pale hatua za uzingatiaji usalama ziwe zimefuatwa ili kuepusha ajali
nyingine.
Kwa upannde wake Mchungaji Nuhu Suleman alie ongoza ibada hiyo ya
kuwaombea marehemu alisema, hapana budi kumshukuru mungu kwa kila
jambo na kila jambo hukusudiwa na mungu. Amewakumbusha waumini
wote kumuelekea mungu kwani yeye ndie mwenye upekee na ufalme na
kwamba maisha ya binaadamu yana ukomo ni vyema kila mmoja
akajiandaa na safari hiyo.
No comments:
Post a Comment