Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Usirika Dkt.
Titus Kamani akiongea na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Hivi
karibuni Jijini Dodoma
Kaimu Mrajis wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Dkt. Benson Ndiege akisisitiza jambo wakati wa kikao na watumishi wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika, Jijini Dodoma
Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao cha Watumishi na Viongozi wa Tume
Bi. Petronila
Shirima akichangia mada wakati wa kikao cha Watumishi
Watumishi
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) wamepewa wito kuwa wabunifu katika maeneo
yao ya kazi kwa kadri ya shughuli na matakwa ya kazi zao. Wito huo umetolewa na
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani tarehe 12 Novemba
2019 wakati wa kikao cha watumishi wa Tume, Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani akiongea katika kikao hicho
alieleza vipaumbele mahususi katika Sekta ya Ushirika ni pamoja na kubadili
Ushirika kuwa katika mlengo wa kibiashara ili mkulima aweze kunufaika zaidi na
mazao anayozalisha. Akitaja ushiriki wa Sekta ya Ushirika katika Uchumi wa
Viwanda ili kuchangia katika kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa kati,
kuongeza idadi na wigo wa wanaushirika katika sekta ya Ushirika nchini,
kuhakikisha uadilifu unaongezeka katika nyanja zote kwa maendeleo ya Sekta ya
Ushirika.
“Tuwe
sehemu ya mabadiliko chanya, Ushirika unatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya
nchi yetu kiuchumi na kijamii. Hivyo, nawaomba watumishi wote wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika katika ngazi zote kutekeleza wajibu na majukumu yenu kwa
weledi na kuzingatia vipaumbele muhimu vilivyo mbele yetu ili kuendeza Sekta ya
Ushirika,” alisema Dkt. Kamani
Kaimu
Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Dkt. Benson Ndiege akiongea na watumishi wa Tume katika kikao hicho, amewataka
watumishi kuwa wabunifu na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia
taratibu za utumishi wa Umma.
“Kila mmoja katika utekelezaji wa majukumu
yake ajaribu kufikiria na kuja na mambo mapya ya kuboresha utekelezaji wa
majukumu yake ili kuhakikisha kuwa anatoa huduma bora katika eneo lake. Hivyo,
kwa pamoja wote tukiwa watu wa kujiongeza basi Sekta ya Ushirika itazidi
kusonga mbele tukikumbuka kwamba huduma bora kwa wananchi ni kipaumbele chetu
siku zote,” alisema Dkt. Ndiege
Pamoja
na mambo mengine, Kaimu Mrajis alisema Changamoto zinaweza kubadilishwa kuwa
fursa endapo wahusika wataamua kwa nia dhabiti ya mabadiliko. Hivyo kwa mtazamo
huohuo aliwaomba watumishi wa Tume kuziona changamoto zilizopo katika Sekta
hiyo kama fursa ya kufanya mabadiliko, kuweka mifumo mipya na ni nafasi ya kila
mtumishi kufanya wajibu wake ili kutekeleza wajibu wa Tume na kutoa huduma bora
kwa Wanaushirika na wananchi wote.
Kwa
upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE tawi la Tume Bw. Mshumba
akichangia maoni ya uboreshaji wa utendaji waTume amesema watumishi wameyapokea
maelekezo na vipaumbele vilivyoelekezwa na wako tayari kutoa ushirikiano wa
dhati katika kuhakikisha Sekta ya Ushirika inaimarika na kuwa endelevu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment