Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekazaji nchini (TIC),
Bw.Geofrey Mwambe akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya TIC kwenye Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekazaji nchini (TIC),
Bw.Geofrey Mwambe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
kuhusu mafanikio ya TIC kwenye Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO).
*****************************
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Kituo cha
Uwekezaji Nchini (TIC) katika kipindi cha miaka minne kuanzia Novemba
2015 hadi Novemba 2019, imesajili jumla ya miradi 1174 yenye thamani ya
Dola za Marekani Bilioni 15,756.9 huku sekta ya viwanda ikiongoza kwa
kutoa asilimia 53 ya miradi yote nchini.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mtendji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC)
Geoffrey Mwambe wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Taasisi hiyo chini ya Utawala wa
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.
Anaongeza kuwa kati yote
iliyosajiliwa nchini, tasnia ya viwanda ina jumla ya miradi 626 huku
miradi mahili yenye uwekezaji mkubwa ikiendelea kuwavutia wawekezaji na
kuzidi kuajiri maelfu ya Watanzania pamoja na kusaidia kupunguza
uagizaji wa bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa kupitia miradi
hiyo, jumla ya ajira zipatazo 159,833 zimezalishwa katika ajira za moja
huku ajira 60,465 zikizalishwa kutokana na ukuaji wa tasnia ya viwanda
nchini na nyingine ikiwemo usafirishaji kutoa ajira (11482), utalii
(7861) na huduma nyinginezo (5376).
‘’Dhamira ya Serikali ya Awamu ya
Tano ni kuongeza masoko ya bidhaa zetu za ndani, na tangu dhamira ya
uchumi wa viwanda itangazwe na Serikali ya Awamu ya Tano tumeshuhudia
ujenzi wa viwanda vingi ikiwemo viwanda vya maziwa katika maeneo
mbalimbali ya nchi na sasa hatuagizi maziwa kutoka Uholanzi na jirani
zetu nchi ya Kenya kama tulivyokuwa tukifanya huko nyuma’’ alisema
Mwambe.
Mwambe alisema ili kufikia malengo
ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kufikia uchumi wa kati kupitia
ujenzi wa viwanda, TIC ilifanya mageuzi na maboresho mbalimbali katika
sera na sheria ya uwekezaji Na. 26 ya mwaka 1997 ili kuhakikisha kuwa
wawekezaji wa ndani nanje ya nchi wanapata fursa ya kushiriki katika
kujenga uchumi.
Kwa mujibu wa Mwambe alisema kuwa
TIC imeendelea kuimarisha mifumo na taratibu mbalimbali za uwekezaji
nchini ambazo awali zilikuwa zikileta usumbufu na vikwazo mbalimbali kwa
wawekezaji, ambapo kwa sasa imeweza kuongeza idadi ya watumishi katika
ofisi hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali.
Akitolea mfano alisema kabla ya
kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, TIC ilikuwa na jumla
ya watumishi 5 kutoka katika Idara mbalimbali za Serikali lakini kwa
sasa kuna jumla ya Maafisa 25 kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi
mbalimbali za Serikali.
‘TIC tumewaweka pamoja maafisa
mbalimbali wa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Umma kwa ajili ya
kurahisisha upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali na sasa kuna
huduma zote za msingi kwa mwekezaji zinazotolewa moja kwa moja katika
dawati letu’’ alisema Mwambe.
Akifafanua zaidi Mwambe alisema
ndani ya kipindi cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano Serikali
imeweza kuanzia viwanda vikubwa kupitia miradi ya kimkakati yenye mtaji
wa zaidi ya Dola 100- 500 za Marekani ambavyo vimetoa ajira lukuki kwa
Watanzania.
Akitolea mfano wa kiwanda cha
kutengeza vigae ‘tiles’ cha Twyford Ltd kilichopo Chalinze Mkoani
Pwani, Mwambe alisema kiwanda hicho kina mtaji wa kiasi cha Tsh Bilioni
130 kimeweza kutoa ajira za moja kwa moja takribani 2000 ambapo
takribani asilimia 90 ya malighafi zake zinazalishwa hapa nchini.
‘Vipo viwanda vikubwa kupitia
wawekezaji mahiri ambao wameweza kuwekeza katika miradi mikubwa ya
kimkakati nah ii imewezekana kutokana na kufanya mageuzi makubwa ya sera
na sharia ya uwekezaji ya mwaka 1997 na sasa uwekezaji wake umeanza
kuleta manufaa makubwa nchini’’ alisema Mwambe.
Aidha aliwataka wawekezaji pindi
wanapopata changamoto mbalimbali wasisite kuwasiliana na ofisi yake kwa
kuwa malengo ya ofisi yake ni kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya
Awamu ya Tano katika kuwavutia wawekezaji nchini.
No comments:
Post a Comment