Mlezi wa Kikundi cha Wake wa
Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa (kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce
Ndalichako (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa
Waziri Mkuu Mstaafu , Mama Tunu Pinda (wa tatu kulia) wakiwapa chakula
watoto wa kituo cha Watoto wenye ulemavu cha Buhangija wilayani
Shinyanga baada ya kukabidhi majengo ya vyumba vinne vya madarasa na
vyoo kumi, Novemba 10, 2019.
Mlezi wa Kikundi cha Wake wa
Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho kilipokabidhi majengo
ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha waotot wenye ulemavu cha
Buhangija wilayani Shinyanga Novemba 10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi
katika makabidhino hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia,
Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta
Mboneko.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizindua madarasa manne ya Kituo
cha watoto walemavu cha Buhangija wilayani Shinyanga yaliyojengwa kwa
ufadhili wa kikundi cha wake wa viongozi cha New Melleanium Women Group.
Wa nne kulia ni Mlezi wa kikundi hicho, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa, Wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mke wa Waziri
Mkuu Mstaafu, Mama Tunu Pinda, kulia ni Mama Hasina Kawawa, wa tano
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko.
Mlezi wa kikundi cha Wake wa
Vingozi cha Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akisalimiana na watoto wa kituo cha walemavu cha Buhangija
wilayani Shinyanga baada ya kikundi hicho kukabidhi majengo ya madarasa
manne na vyoo kumi kwa shule hiyo, Novemba 10, 2019. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack
Mlezi wa kikundi cha wake wa
Vingozi cha New Millennium Group, Mke wa Waziri mkuu, Mama Mary Majaliwa
akikumbatiana na Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Mama Tunu Pinda, Mke wa
Waziri Mkuu Mstaafu katika hafla ya kukabidhi majengo ya madarasa manne
na vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Walemavu cha Buhangija wilayani
Shinyanga yaliyojengwa kwa ufadhili wa kikundi hicho, Novemba 10, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment