Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI Seleman Jafo amewaagiza
wasimamizi wa uchaguzi kuanza kupokea ratiba za kampeni kutoka katika
vyama vya siasa nchini kuanzia leo hadi kesho jioni .
Aidha,amesema tarehe ya matukio na
shughuli zingine zote zinazohusu uchaguzi huo zitaendelea kwa mujibu wa
kanuni za uchaguzi serikali za mitaa wa mwaka 2019
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo
jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa
taarifa ya wa taarifa ya wagombea waliorejesha fomu ,uchukuaji
fomu,uteuzi,pingamizi na rufaa lililoanza tarehe 29/10/2019 hadi tarehe
9/11/2019.
Jafo amesema jumla ya waliorejesha
fomu ni jumla ya wananchi 539,993 sawa na asailimia 97.3 kati ya
wananchi 556,036 wote waliochukua fomu.
Aidha ametaja orodha ya vyama
vilivyochukua na kurejesha fomu ambapo wagombea kutoka CCM walikuwa
412,872 sawa na asilimia 74,CHADEMA walikuwa 105,937 sawa na asilimia
19,CUF walikuwa 24,592 sawa na asilimia 4,ACT-Wazalendo walikuwa 8,526
sawa na asilimia 1.5,NCCR-Mageuzi walikuwa 2,244 sawa na asilimia
0.4,na vyama vingine vyenye usajili wa kudumu walichukua chini ya
asilimia 0.1 kwa kila chama.
Hata hivyo waziri Jafo amesema
katika zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kulikua na changamoto kwa
wagombea wengi kufanya makosa mengi ya kikanuni yaliyopelekea wengi wao
kutoteuliwa.
No comments:
Post a Comment